- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Limefanyika zoezi kabambe la kufanya usafi wa mji likiongozwa na katibu wa CCM Wilaya Bi Anastazia A Amas, katibu wa wazaziWilaya Comred Abdalah kirobi katibu itikadi na uenezi Wilaya Comred Damian Godian, Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Ngara Ambaye ni katibu wa Mbunge Ndg Ernest B Joseph, Mkiti Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara, wah Madiwani Ngara Mjini ,kabanga, Mkuu wa Kitengo Cha usafi na mazingira Ndg Yasin Mwinory, Afisa Tarafa Nyamiaga Ndg Jawadu Yusuph Afisa utamaduni michezo wilaya, wananchi pamoja na viongozi wa chama na serikali.
Zoezi hilo la Usafi kabambe limefanyika kuelekea Kilele Cha maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa Kwa chama Cha Mapinduzi.
Maeneo Yaliyofanyika usafi na viongozi wa chama ,Serikali na Wananchi ni sokoni Ngara Mjini, Barabara Kuu Ngara Mjini, ofisi za CCM Wilaya, Barabara ielekeayo Murgwanza, uwanja posta, ikiwa na kusafisha Mitaro ya Barabara,kufyeka Nyasi,kufagia na kuokota uchafi kama vile chupa, karatasi , vocha zilizotumika nk.
Katibu wa CCM Wilaya Bi Anastazia amewashukuru wote walioshiriki zoezi la Usafi kabambe wanaccm, Serikali na Wananchi Kwa kuungana pamoja kufanya usafi ikiwa ni kuelekea Kilele Cha maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa Kwa CCM.
Aidha amewaambia zoezi la Usafi ni Endelevu wilayani Ngara tuendelee kufanya usafi Kila siku ya alhamisi ikiwa ni kuunga mkono Jitihada za viongozi wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J. Kahabi, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg. Solomon O Kimilike walipozindua zoezi la Usafi kwa Wilaya nzima kata ya Rusumo Tarafa ya Nyamiaga wilayani Ngara.
Zoezi la ufanyaji usafi sokoni Ngara mjini.
Zoezi la Usafi kufagia Barabara akiwemo Mhe Diwani Ngara mjini.
Mkuu wa Kitengo Cha Afya usafi na mazingira Ndg Yasin Mwinory akiwa na Afisa utamaduni michezo pamoja na wafanya usafi usafi baada ya kumaliza kufanya usafi.
Katibu wa CCM Wilaya Comred Anastazia A Amas Akiongoza zoezi la Usafi ofisi za CCM Wilaya baada ya kumaliza maeneo Mbalimbali ya Ngara mjini.
Katibu CC M Wilaya akiongoza zoezi la kufyeka Nyasi Ndefu eneo la ofisi za chama Cha Mapinduzi wilaya.
Mhe diwani Ngara Mjini akiwa kwenye zoezi la Usafi wa pamoja.
Zoezi la Usafi Comred Abdalah kirobi katibu wa Jumuiya ya wazazi Wilaya akiwa na Diwani Ngara mjini Mhe Kennedy Festo wakisafisa Barabara ielekeayo ofisi za Mhe mkuu wa wilaya.
Afisa Tarafa Nyamiaga Ndg Jawadu Yusuph akiwa na katibu wa Jumuiya ya wazazi na Wananchi kufanya usafi.
Zoezi la Usafi sokoni.
Mji ni msafi wa Ngara mjini.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa