- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Saturday 21st, December 2024
@Uwanja wa Halmashauri - Ngara mjini
Mafunzo ya Michezo yaliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Ngara yamefanyika Wilayani kuanzia Tarehe 23/04-30/04/2023 .
Mafunzo hayo yalishirikisha walimu 52 kutoka MANSPAA ya Bukoba, Halmashauri za kyerwa,Karagwe,Biharamulo,Muleba na Ngara.Ambapo Ndg Kepha Elias Afisa michezo mkoa, Ndg Said Salum Afisa Michezo Utamaduni wilaya , Bi Elina Patruce Afisa utamaduni Michezo Wilaya walishiriki katika mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yalifanyika Kwa nadhalia na vitendo (Theory and Practical) Kwa michezo ya Netball, Volleyball, Basketball,na Handball ambapo yaliwezeshwa na wakufunzi Mahili wa kitaifa.
Mgeni Rasmi alikuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji Constantine Msemwa ambapo alitoa vyeti Kwa washiriki ,Aidha aliwataka Wana mafunzo kwenda kufundisha michezo ipasavyo Shuleni Ili kufanya vizuri katika mkoa wetu kwenye mashindano ya Umitashumta na Umisseta Ngazi yaTaifa. Mwisho aliwashukuru wakufunzi Ndg Christopher Eliakim na Ibrahimu yunga Kwa kufundisha Kwa umahili mkubwa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa