- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
21/01/2026
Mhe Wilbad Bambara Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ameiongoza kamati ya Fedha,utawala na Mipango kukagua miradi ya maendeleo . Akiongozana na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya ,Waheshimiwa Madiwani baadhi ambao ni wajumbe , wataalam wa Halmashauri pamoja na katibu wa Mbuge wa Jimbo la Ngara.
Miradi ya Maendeleo liyotembelewa ni
1/ Ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shule ya Msingi Kasharazi wenye gharama ya Tsh Milion 101,000,000/=fedha toka BOOST
2.Ukamilishaji wa chumba cha Maabara Rusumo B Sekondari Tshs Milioni 25,000,000/= fedha toka SEQUP
3.Ukamilishaji wa Zahanati ya Kabulanzwili Tsh Milion 60,000,000/= fedha toka Serikali Kuu jengo hatua ya umalizaji
4.Mradi wa Kikundi cha vijana -AMUA Cha kutengeneza Sabuni mkopo wa tsh Milion 10,000,000/= fedha toka mapato ya Ndani kikundi hicho
Marejesho yanaendelea.
5.Mradi wa Ujenzi wa shule ya msingi mpya kata ya kasulo eneo mkabala na Shule ya Sekondari Rusumo gharama tsh Milion 330,700,000/= toka BOOST na Tsh Milion 25,000,000/= toka Serikali kuu.
Ziara hiyo ya kamati ya Fedha,Utawala na Mipzngo kutembelea Miradi Mbalimbali itaendelea tarehe 22/01/2026

Ujenzi wa shule ya Msingi Mpya kata ya kasulo

Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi kata ya kasulo

Madarasa shule mpya ya msingi kata ya kasulo

Ujenzi wa vyumba 4 shule ya Msingi Kasharazi

Madawati ya Shule ya msingi Kasharazi kata ya Rusumo

Zahanati ya Kabulanzwili kata ya Rusumo

Ndani chumba cha maabara shule ya Sekondari Rusumo

Walipotembelea kikundi cha kutengeneza sabuni - AMUA

Sabuni zilizotengenezwa na kikundi cha AMUA
Sabuni
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa