- Mwanzo
 - Kuhusu sisi
 - Utawala
 - Fursa za uwekezaji
 - Huduma zetu
 - Madiwani
 - Miradi
 - Machapisho
 - Kituo cha Habari
 
| 
				 Eustach Ntayandi 
			 | 
			
				 | 
			
				 CHEO 
			 | 
			
				 | 
			
				 MAWASILIANO 
			 | 
		
|                            
				 | 
			
				 | 
			
				 District Information, Communication and Technology Officer (DICTO) 
			 | 
			
				 | 
			
				 +255 769 587 228 
				ictsupport@ngaradc.go.tz 
			 | 
		
	
Kitengo cha Technolojia ya habari na mawasiliano na uhusiano ni moja ya vitengo vipya vya Halmashauri ya wilaya ya Ngara vilivyoanzishwa mwaka 2011. Kitengo kinashughulikia mambo makuu yafuatayo:-
Eneo la TEHAMA
• Kusimamia ufungaji na kujaribu vifaa vyote vya elektroniki vilivyoko halmashauri.
• Kutumia na kuhifadhi programu za kompyuta, vifaa vya kompyuta na mitambo ya mifumo na mawasiliano;(kama simu, intanet, kanzidata na vitu vingine).
• Kusimamia shughuli zote za matengenezo ya vifaa vya elekroniki pamoja na kompyuta.
• Kuhakikisha mifumo ya TEHAMA iliyopo katika Halmashauri inafanya kazi kama inavyotakiwa;
• Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumishi wote wa Halmashauri katika eneo la TEHAMA;
• Kutoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri katika masuala ya TEHAMA zikiwemo programmu mbalimbali;
• Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA;
• Kuibua mahitaji ya mifumo ili iweze kusanifiwa na kisha kutengenezwa na kutumika;
• Kuchambua na kuainisha huduma zinazoweza kutolewa na mifumo ya kielekroniki katika Halmashauri;
• Kuhakikisha miundombinu kiambo (Local Area Network) katika Halmashauri inafanya kazi na mtandao wa intaneti unapatikana;
• Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kuteleza kazi za TEHAMA katika Halmashauri;
• Kutengeneza utaratibu mzuri wa kutunza taarifa na data ili ziweze kutumika wakati wa majanga;
• Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vyote vya TEHAMA;
• Kutafiti na kuchambua matatizo ya vifaa vya TEHAMA na kutoa suluhisho;
• Kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa TEHAMA wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo;
• Kutoa specification za vifaa kwa ajili ya manunuzi;
• Kushiriki katika zabuni za vifaa vya TEHAMA na kuhakiki ubora wake kabla havijaanza kutimika; na
• Kuhakikisha Halmashauri ina tovuti na inapatikana wakati wote.
	
Eneo la Uhusiano
• Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa kazi za Uhusiano;
• Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kuteleza kazi za Uhusiano katika Halmashauri;
• Kutangaza kazi na miradi inayofanyika katika Halmashauri;
• Kutangaza maeneo ya uwekezaji ya Halmashauri katika tovuti, radio na majarida;
• Kuhakikisha tovuti ya Halmashauri ina taarifa mpya kila wakati pamoja na District Profile;
• Kuandaa na kutoa majarida kuhusu Halmashauri;
• Kushiriki katika mijadala ya jamii kuhusu masuala ya Halmashauri;
• Kutumia TEHAMA katika kutoa elimu kwa jamii;
• Kusimamia press briefing za Halmashauri;
• Kushauri Halmashauri juu ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa nyaraka kwa wadau mbalimbali; na
• Kushirikiana kwa karibu na afisa uhusiano wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo.
• Kuratibu habari za Halmashauri na kuzitoa kwa wahusika kwa mujibu wa kanuni za kitengo cha habari.
• Kuandaa, kuandika na kuhakiki machapisho, makala na miswada mbalimbali ya halmashauri, pamoja na kalenda.
• Kuwa kiungo kati ya maeneo mengine ya kituo cha data, programu na mawasiliano ya kompyuta.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa