- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
22/01/2025
Kamati ya fedha ,Utawala na Mipango leo imendelea na ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo Wilaya ya Ngara, ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Theophilda William, kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri pia timu hiyo ikiwa na waheshimiwa Madiwani pamoja na wataalam kutoka Halmashauri.
Miradi ya Maendeleo iliyotembelewa na kukaguliwa ni
1. Ujenzi wa nyumba ya mwalmu shule ya msingi Gashaza kata ya Muganza gharama Tsh 51,000,000/= fedha toka (GPE LANES)
2. Umaliziaji wa ujenzi wa zahanati ya Nyabihanga kata ya Bukiriro gharama ya Tsh Milion 95,000,000/= kupitia fedha ya fidia ya ardhi ya Vijiji toka Tembo nickel,
3. Ukamilishaji wa zahanati ya Murulama kata ya Bukiriro gharama Tsh Milion 60,000,000/= fedha toka serikali kuu.
4. Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Kabanga kata ya Kabanga gharama ya mradi ni Tshs. 88,600,000/= fedha kutoka BOOST.
5. Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), kichomea taka, shimo la majivu, placenter pit na uzio wake pamoja na umaliziaji wa jengo la maabara Zahanati ya Kanazi kwa gharama ya Tshs.250,000,000/=fedha toka serikali kuu
6. Ujenzi wa Shule mpya ya mchepuo wa kiingereza Nakatuga Ngara mjini gharama ya Mradi tsh Milion 305,000,000/= fedha toka mapato ya ndani
7. Ukamilishaji wa chumba cha maabara Shule ya Sekondari Ngara fedha kutoka serikali kuu kiasi cha Tshs 30,000,000/=
8. Ujenzi wa ukumbi wa FATMA MWASSA Ngara mjini gaharama hadi sasa tsh 273,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani.
9. Kikundi cha kabanga Matunda kilimo cha parachichi waliopewa mkopo wa tsh 40,000,000/= fedha toka mapato ya Ndani.

Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Gashaza kata ya Muganza

Ujenzi wa Zahanati ya Nyabihanga kata ya Bukiriro

Ukamilishaji wa Zahanati ya Murulama kata ya Bukiriro

Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa na Matundu 6 ya vyoo Shule ya Msingi Kabanga

Ujenzi wa kituo cha afya Kanazi

Uendelezaji wa ujenzi wa Maabara kituo cha afya kanazi

Ujenzi wa Shule Mpya ya Mchepuo wa Kiingereza Nakatunga Ngara Mjinj

Ukamilishaji wa Chumba cha Maabara Shule ya Sekondari Ngara

Ndani ya Chumba cha Maabara Ngara Sekondari

Ujenzi wa Ukumbi wa FATMA MWASSA wa kisasa wa Halmashauri fedha za mapato ya ndani.

Ukumbi wa FATMA MWASSA unaojengwa Ngara Mjini
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa