- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
15/04/2025
Kampeni hiyo iliyozinduliwa Mkoa wa kagera tarehe 14/04/2025 na Waziri wa sheria na Katiba Mhe Dr Damas Ndumbaro Mjini Bukoba zoezi linalotekelezwa kwa wilaya zote za Mkoa wa Kagera.
Kampeni hii inatokana na Azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuimarisha mfumo wa kutatua changamoto zunazowakabiri wananchi bila kusubiri kuwasilisha changamoto wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa.
Ilielezwa Lengo la kampeni kulinda Kukuza na kuimalisha upatikanaji wa haki kwa watu wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria.
Aidha katika wilaya ya Ngara zoezi hili linaanza tarehe 15/04/2025 hadi 23/]4/2025. ambapo Jumla ya kata 10 vijiji 30 watafikiwa.
Kata zitakazotembelewa ni Bugarama, Rulenge, Muganza, Murusagamba, Nyakisasa, Rusumo,
Kasulo, Murukulazo, Kabanga na Ngara mjini.
Wataalam watakaohusika katika utekelezaji wa kampeni ni Mratibu kutoka wizara ya katiba na sheria, Afisa maendeleo ya Jamii, Mwanasheria wa Hamashauri, Afisa Ardhi, Mwanasheria kutoka chama cha Tanganyika , Afisa dawati Jinsia,Afisa ustawi wa Jamii,Wasaidizi wa kisheria, Maafisa toka dawati la msaada wa kisheria na Mwandishi wa Habari
Leo wamefika ofisi ya Mhe Col Mthias J kahabi Dc pia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kujitambulisha na kuanza kazi hiyo.
Aidha Ndg Emmanuely kulwa mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ambaye kaimu DED anawaalika wananchi wenye changamoto wafike watasaidiwa.
Naye Mhe Col Mathias J kahabi Dc Ametoa wito kwa wananchi kufika katika maeneo hayo yatakayotembelewa na wataalam kupata elimu ya sheria pamoja na huduma ya Msaada wa kisheria kwenye maeneo yote ya migogoro ya ardhi .mirathi, ukatili ndoa nk. wajitokeze kwa wingi kupata huduma hii inayotolewa kwa wananchi bila gharama. Alimalizia kwa kumpongeza Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha utaratibu wa kuwasaidia wananchi.
Timu hiyo ilipofika pia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa