- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara - 24/12/2025,
Mkuu wa wilaya Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya walifanya ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania na Rwanda ambao unatenganishwa na mto Kagera kama unavyooneka kwenye picha.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia usalama wa mpaka na kuongea na wananchi wanaoishi jirani na mpaka huku akiwasisitiza kulinda mpaka wetu na jirani zetu.
Aidha, alikagua vipenyo ambavyo sio rasmi na vinatumika na wananchi wa pande zote mbili kuingia na kutoka nchini bila kufuata taratibu na sheria za Nchi za Uhamiaji.
Amewataka Wanajeshi wetu(JWTZ) walioko kwenye viteule kwa shughuli za ulinzi na usalama wa mpaka kushirikiana na Viongozi wa vijiji pamoja na wananchi wote walioko mpakani kudhibiti hali hiyo na kuhakikisha wanatoa taarifa kwa Mamlaka husika endapo kuna wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufuata sheria za nchi.
Ziara ya Mhe DC Kahabi ni endelevu ambapo pia anafuatana na Meneja wa TARURA Wilaya na Watendaji wa ofisi yake kuona maeneo yenye changamoto katika barabara mhimu za Kiusalama kuelekea mpakani na akapongeza kazi nzuri inayofanywa na TARURA Wilaya japo bajeti ya matengenezo ya barabara hizo za Kiusalama ni ndogo ukilinganisha na mahitaji.

Ngara Kazi ya ulinzi na usalama inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa