- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi leo tarehe 15/4/2025 amezindua rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Uzinduzi huo imefanyika katika Kijiji cha Bugarama, Kata ya Bugarama ambapo timu ya Watalaam wa Sheria toka Wizarani, Mkoani na Wilayani Aidha watazunguka katika Kata 10 na Vijijini 30 vya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa lengo la kutoa ushauri wa Kisheria na pia kusikiliza na kutatua Kero za wananchi kuhusu changamoto zinazowakabiri kwenye jamiii ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, vitendo vya ukatiri wa kijinsia, haki za binadamu na mengine mengi.
Pichani ya pamoja Mhe. DC Ngara Mhe Col Kahabi akiwa na wazee maarufu wa Kijiji cha Bugarama Pamoja na wadau wa maendeleo ambao walifika kutoa pongezi kwa Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzia hii Kampeni ya Msaada wa Kisheria mahsusi kwa ajili ya wananchi wa kawaida ambao hawana msaada wowote wa kumaliza Kero na Changamoto za masuala ya kisheria.
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa