- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
25/08/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi na shughuli za Mwenge wa Uhuru. Akifuatana Bi Hatujuani Ally Lukari Katibu Tawala Wilaya, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Mwl Said Salum Ambaye ni Mratibu wa Mwenge , Eng Simon Mtuka Mhandisi wa ujenzi wilaya, Ndg Said Nampala kutoka ofisi TAKUKURU Wilaya na Afisa Afya Wilaya.
Timu hiyo ikiongozwa na Mhe Col Kahabi imetembelea na kukagua
Miradi ya Mwenge wakianza na
1 Eneo la Mapokezi uwanja wa Baramba / lukole - K9
2.Nishati safi na salama
3.Shule Ya Amali - kasharazi
4.Mradi wa Maji -kumuyange
5.Ukumbi wa Kisasa Fatma Mwassa - Ngara Mjini
6.Shule ya Mchepuo wa kiingereza ya Halmashauri - Nakatunga
7.kituo cha Afya kanazi - Maeneo ya Vibanda vya Mapambano dhidi ya Malaria, UKIMWI, uchangiaji Damu salama, ukatili wa kijinsia na Lishe
8 Eneo la Stand kabanga utakapotolewa ujumbe wa Mwenge
Pia vibanda vya apambano dhidi ya Rushwa, Dawa za kulevya na Uchaguzi
9.Mradi wa uwekezaji vijana Matunda -Ibuga Kabanga
10.Ujenzi wa Daraja la Mkajagali Kumwendo
11. Eneo la Mkesha( Uwanja wa Mpira Rulenge )
12. Eneo la Kongamano na vibanda vya biashara kwa wananchi
Timu imepongeza kwa Juhudi zinazoendelea, Aidha Maelekezo na ushauri Mbalimbali umetolewa kwa kila Mradi
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa