- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
10/09/2025
Mkuu wa Wilaya ya Col. Mathias J Kahabi amewaita wananchi wote wa NGARA kujitokeza kwa Wingi katika Mapokezi ya Mwenge wa uhuru kwenye Miradi na Mkesha Kabambe wa Mapokezi Uwanja wa Baramba- Lukole High School usiku wa kuamkia Sepitemba 13 na kuushangilia maeneo yote utakapopita kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali iliyopangwa.
Mwenge wa uhuru utapokelewa ukitokea Wilaya ya Karagwe ambapo utakimbizwa umbali wa kilometa 74 ukianza na Mradi wa Nishati safi eneo la mapokezi, Jiwe la Mradi wa maji kumuyange kata ya Nyamiaga , kuona kiwanja cha Michezo ngara mjini, jiwe la msingi shule ya mchepuo wa Kiingereza Nakatunga ,Jiwe la msingi kituo cha afya Kanazi ( jengo la OPD). Ujumbe wa mwenge kabanga stendi,kutembelea Mradi wa uwekezaji Vijana Ibuga Kabanga na Daraja la kumwendo , kata ya Mbuba
Mkesha utasindikizwa na Burudani kabambe wakiwepo wasani kutoka nje na Ndani.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa