- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Leo tarehe 25/8/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amekutana na Maafisa wanafunzi wa Kijeshi toka Chuo cha Kijeshi Monduli ambao wako katika mafunzo ya vitendo katika Makao Makuu ya viteule vya JWTZ, 23KJ yaliyopo K9.
Mkuu wa Kiteule cha K9, Maj Raphael Paschal amepongeza ziara ya Mhe DC Ngara Col Kahabi na kusema Maafisa wanafunzi idadi saba(7) wakiongozwa na Mkufunzi wao Luteni Julius R. Kahabi wamejifunza mambo mengi ya kiulinzi na usalama wa mipaka ya nchi yetu hususan mpaka wetu wa Kaskazini Magharibi na jirani za Burundi na Rwanda.
Luteni Julius Kahabi Mkufunzi na Mkuu wa Msafara huo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Kijeshi Monduli Maj Gen Mwaseba ametoa pongezi nyingi kwa ushirikiano mkubwa walioupata yeye na wanafunzi wake kwa muda wa mwezi mmoja walipokuwa kwenye mafunzo ya vitendo kuanzia Makao Makuu ya Kikosi 23KJ Biharamulo, Makao Makuu ya viteule K9 na Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Ngara.
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa