- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Tarehe 23/12/2024, DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi akifuatana na Mwl Amani Bihondwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Solomon Kimilike wametembelea Mradi wa shule ya Secondary ya Amali - Kasharazi, Kata ya Rusumo na kuridhishwa na maendeleo mazuri ya mradi huo ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia 80.
Mradi huu mkubwa wenye thamani ya Tshs bilioni 1.6 una Miundombinu mbalimbali kama ifuatavyo;-
1. Jengo la Utawala
2. Vyumba vinane(8) vya madarasa
3. Vyumba viwili(2) vya maabara
4. Jengo la TEHAMA
5. Jengo la Maktaba
6. Matundu manane(8) ya vyoo
7. Nyumba moja ya Mwalimu
8. Mabweni manne(4)
9. Karakana ya Uashi
10. Karakana ya Umeme
11. Bwalo moja
12. Viwanja viwili(2) vya michezo
13. Kisima cha maji chini ya ardhi
Aidha, Mhe Col Kahabi DC Ngara kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hii anapenda kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa Mhe Dr Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Ngara Kazi inaendelea....
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa