- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 28/7/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, viongozi wakuu wa idara mbalimbali za Serikali zilizopo mpakani Rusumo pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata Rusumo walikutana na kufanya Kikao kazi maalum.
Lengo la Kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kumaliza changamoto chache zilizopo mpakani hapo ikiwemo kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu, kudhibiti biashara haramu ya magendo, kuimarisha zaidi mahusiano mazuri yaliyopo baina yetu na nchi jirani pamoja na suala la Usalama wa mpaka.
Wajumbe walijadiliana na kuweka mikakati ya pamoja. Aidha, vikao hivi ni endelevu na Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara amesisitiza lazima tusimame imara kuhusu Usalama wa mpaka wetu kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Ngara kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa