- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 27/8/2025, DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi amefanya Kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya ambapo yeye na Viongozi wenzake wamejadiliana mambo mbalimbali kuhusu kuboresha mazingira ya ukusanyaji Kodi, kudhibiti biashara haramu ya magendo kupitia mipaka yetu na nchi jirani pamoja na utoaji elimu kwa wafanyabiashara kulipa Kodi bila shuruti, matumizi ya mashine za EFD pamoja na changamoto zinazowakabiri wafanyabiashara wetu katika maeneo yao ya biashara.
Aidha, Viongozi mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa H/W Ngara ndg Solomon Kimilike, Meneja TRA Wilaya Ndg Victor Kibasa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wilaya Ndg Crispin Kamugisha, Katibu tawala wa Wilaya Bi. Hatujuani Lukari, wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya na wajumbe wengine wa Kamati hiyo walitoa ushauri na hatimaye maazimio kuhusu namna ya kumaliza changamoto zinazowakabiri wafanyabiashara na mikakati ya pamoja ya kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato Wilayani Ngara.
Ngara Kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa