- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 23/7/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara ametembelewa na Maafisa wakuu pamoja na Maafisa wadogo toka Makao Makuu ya Jeshi - Dodoma na wengine toka Makao Makuu ya Jeshi la nchi kavu - Kibaha, Pwani.
Maafisa wakuu na Maafisa wadogo hao ni pamoja na Col HS Lyambilo, Col HM Komba, Col ES Massawe, Lt Col EE Mpindasigulu, Maj JJ Mvula, Capt RT Maunga, Capt LA Mwanfundile na mwenyeji wao Maj Raphael Paschal Mkuu wa Kiteule cha K9 - Ngara.
Leo la ziara ya Viongozi hao ni pamoja na kukagua hali Ulinzi na Usalama unaofanywa na Maafisa na askari walioko katika mpaka wetu na nchi jirani.
Aidha, wakuu hao wakitoa maelezo kwa Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara waeleza kuwa wanaridhishwa na hali ya utayari na utimamu wa Kijeshi uliopo kwa Makamanda na Wapiganaji toka viteule vya JWTZ walioko mpakani kwa jukumu mahsusi la ulinzi na Usalama wa mpaka wetu.
Wakuu hao kabla ya kuja Mkoa wa Kagera, Wilayani Ngara wametokea Mkoa wa Kigoma na baada ya Mkoa wa Kagera wataendelea na ziara yao kwenye Mikoa mingine.
Ngara kazi ya Ulinzi na Usalama inaendelea vema na mipaka yake na nchi jirani ni shwari.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa