- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Leo tarehe 07/2/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Burigi - Chato afande Adewa na Maafisa wandamizi ya Hifadhi hiyo, Watalaam toka idara ya Kilimo Wilaya, Viongozi wa Kata ya Kasulo, Viongozi wa Serikali ya kijiji cha Rwakaremela pamoja na wananchi walioathiriwa mazao yao na Tembo toka Hifadhi ya Burigi - Chato(Ngara) wamefika katika Kijiji cha Rwakaremela kwa ajili ya kukagua uharibu mkubwa uliofanywa na Tembo kati ya tarehe 04 na 05/2/2025.
Kundi la kubwa la Tembo linalokadiriwa kufikia tembo 72 liliingia kwenye mashamba ya mahindi na migomba na kufanya uharibu huo usiku wa kuamkia tarehe 05/2/2025 ambapo hasara kubwa imesababishwa na wanyama kwa upande wa Mazao ya Wananchi ndizi na Mahindi.
Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara baada ya kujionea hasara hiyo amwagiza Mhifadhi Mkuu Burigi - Chato kudhibiti hali hiyo na kwamba changamoto kama hizo zisiendelee kujitokeza mara kwa mara kama ilivyo hivi sasa.
Aidha, DC Kahabi akawaagiza Watalaam wa Kilimo na Afisa mazingira kufanya tathmini ya hasara hiyo ili wananchi walioathiriwa na Tembo waweza kupata stahiki yao ya kifuta jasho.
Naye Mhifadhi Mkuu Burigi - Chato ameahidi kuyafanyia kazi maagizo na Mhe DC Ngara na kwamba watashirikiana na Viongozi wa Kata/Vijiji pamoja na wananchi wanaozunguka Hifadhi hiyo kumaliza kero hizo.
Mhe Col Kahabi Dc Ngara akiwa na Askari wanyama pori
Mhe Col Kahabi akiangalia na wananchi mazao yaliyoharibika.
Ngara kazi inaendelea.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa