- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ushirikiano Tanzania, Morocco kuimarishwa
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi inayolenga kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Nishati.
Akiwa nchini humo, Dkt. Biteko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati.
Mara baada ya kuwasili, Dkt. Biteko amepokelewa na Naibu Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu nchini humo, Mhe. Mohamed Ouhmed, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa nishati vijijini (REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa