- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ili uweze kujisajili katika Mfumo wa Wadau wa Sanaa AMIS fuata Link sanaa.go.tz kisha unahitaji kuwa na namba ya NIDA, TIN Namba na Barua Pepe/Email; baada ya kujaza taarifa binafsi
Utatumiwa link kwenye barua pepe na kutengeneza nywila/password yenye mchanganyiko mfano Sanaa@2022 kisha utaingia kwa barua pepe na nywila uliyotengeneza.
Viambatisho vinavyohitajika katika usajili kwenye mfumo
ENEO LA BURUDANI, SHEREHE/KUMBI (Bar, Lounge, Pub, Night Club, Maeneo ya wazi yaSherehe/Burudani nk)
1. Picha za eneo la burudani/sherehe/kumbi muonekano ndani na nje
2. Kibali cha mara ya mwisho (PDF) kwa wanaohuisha vibali
3. Kwa wasajiliwa wapya - fomu ya ukaguzi
Wafanyabiashara ambao hawajasajili jina BRELA, Taasisi, Vyama, Mitandao ya Wasanii na Mashirikisho
NB: Kwa Wafanyabiashara wa kazi za sanaa - ambatisha leseni ya mwisho ya biashara na uwasilishe ombi
Wasajiliwa waliobaki wataweka viambatisho;
1. Katiba (PDF)
2. Picha za viongozi (PDF)ziwe katika ukurasa mmoja na majina yao na vyeo chini ya picha
3. Kibali cha mara ya mwisho (PDF) kwa wanaohuisha vibali
Wafanyabiashara wa Kazi za Sanaa na Kampuni zenye usajili BRELA
1. Namba ya usajili wa Jina/Kampuni BRELA
2. Ingia sehemu leseni nyingine/other licence jaza taarifa husika na kuwasilisha
Vikundi vya Sanaa
1. Katiba (PDF)iwe imesainiwa
2. Picha za viongozi (PDF)
3. Kibali cha mara ya mwisho (PDF) kwa wanaohuisha vibali
4. Orodha ya wanachama ina sehemu ya kujazwa kwenye mfumo
Msanii binafsi
1. Wasifu au CV (PDF)
Kwa kupata ufafanuzi zaidi Tafadhali wasiliana kwa namba hizi za BASATA
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa