- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kujikusanya kujenga miundombinu shuleni, ili watoto 256 ambao hawajapata nafasi waweze kuendelea na masomo yao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Samsoni Mwesiga, amesema hayo ofisini kwake Disemba 21, 2018, kwamba wanafunzi waliofanya vizuri lazima wote waendelee na masomo.
“Watoto waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari Januari 2019 ni 4,203 sawa na asilimia 94.24%, ambapo kati yao wavulana na 2,008 na wasichana ni 1,196; kati yao wanafunzi 256 hawajapata nafasi.” Alisema Ndugu Mwesinga.
Watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 5,066 sawa na 99.5%, kati yao wavulana 2,270 na wasichana 2,696; huku watahiniwa ambao hawakufanya mtihani ni 27 sawa na 0.5%; wavulana 19 na wasichana 08.
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kwamba watahiniwa wavulana waliofaulu ni 2,098, sawa na 88.67%, ambapo wasichana waliofaulu ni 2,362 sawa na 87.51%; huku wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za bweni kawaida, ufundi na ufaulu mzuri ni 18; wavulana 12 na wasichana 06.
Watahiniwa waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kidato cha kwanza kutwa Januari 2019 ni 4,186 sawa na 94.24%, ambapo wavulana ni 1,996 na wasichana 2,190; huku akisema kwamba mwaka 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, ilikuwa na watahiniwa 5,095 waliosajiliwa kufanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi.
Aidha, amesema mwaka 2017 waliofaulu ni wanafunzi 3026 sawa na 80%, ambapo kati yao wavulana walikuwa 1,838 na wasichana 1,980; cha kufurahisha wanafunzi wote walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika chaguo la kwanza.
Ameishauri serikali wakati Halmashauri inaweka miundombinu inayotakiwa kuwastahilisha wanafunzi, ambao hawajapata nafasi kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, serikali ifanya taratibu za kupata walimu, kulingana na idadi ya wanafunzi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa