• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Jisajilini Katika Vikundi Mkopesheke Mjikwamue Kiuchumi: Brig. Jen. Gaguti

Wakati ilipowekwa: January 21st, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti, amewataka Bodaboda Mkoani Kagera, kujisajili katika vikundi, ili watambulike na kupitia vikundi hivyo, wapate mikopo na elimu ya ujasilamali, ili waongeze kipato chao.

Brig. Jen. Gaguti ametoa rai hiyo baada ya kukutana na Bodaboda katika Ukumbi wa Linas Night Club ulioko Manispaa ya Bukoba Januari 17, 2019,  na kuweka wazi ni jinsi gani, atasimamia mikakati yake, ili wafanye kazi zao kama anavyotamani, lakini wakizingatia taratibu na sheria za Usalama Barabarani.

“Nimewaiteni katika mkutano huu nia yangu ni kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi zenu, kwani mnafanyakazi katika mazingira yasiyokuwa mazuri, mkivutana na vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la Polisi wanapotekeleza majukumu yao.” Alitaja Lengo la Mkutano Mkuu wa Mkoa Gaguti

Mkuu wa Mkoa Gaguti aliyataja mambo makuu matatu muhimu ambayo Bodaboda wanatakiwa kuyatekeleza haraka kwanza, Kuunda vikundi na kuvisajili vikundi hivyo katika maeneo yao ya kazi, ili Bodaboda watambulike na kupitia vikundi hivyo wapate mikopo nje ya kuendesha Bodaboda, ili kuingiza kipato zaidi.

Pili, Bodaboda wote wapewe elimu ya Usalama Barabarani, lakini washiriki katika Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kagera; kwani kumekuwa na tabai ya majambazi kujificha katika kazi ya kuendesha Bodaboda, huku wakifanya uhalifu.

Tatu, anataka Bodaboda wapate elimu ya ujasiliamali mbali, ili vijana watarajirike kupitia ujasiliamali pia. “Hivi utafanya kazi hii ya Bodaboda mpaka uzee wako? Ni lazima tuwaandae kuanza ujasiliamali, ambao hata ukizeeka au kupata ajali, hutapata shida na familia yako itaendelea kupata huduma.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Kuanzia sasa hataki kuona au kusikia tena mivutano ya Bodaboda na Jeshi la Polisi; bali wawe na mahusianao mazuri, na kama mfumo anaoulenga utafanya kazi, kutakuwa hakuna haja ya Jeshi la Polisi kuwakamata Bodaboda, bali wao wenyewe wachukuliane hatua mmoja wao anapovunja sheria.

“Hivi karibuni katika Mkoa wa Kagera utalii unaanza, na katika mji wetu wa Bukoba Bodaboda bado wapo ovyo; lakini natamani Bodaboda nyinyi muwe mfano kwa kuvaa sare na kutoa huduma bora za usafiri, ili mikoa mingine waone jinsi vijana wanvyofanya kazi ya Bodaboda, kwa weledi na kufuata sheria.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuongea na Bodaboda Mdau wa Usalama Barabarani Mkoani Kagera Bw. Winston Kabantega, alimesema biashara ya Bodaboda, ilianzia mjini Bukoba, lakini Mkoa huo haumo katika mikoa mitatu bora, inayofanya vizuri katika biashara hiyo nchini.

Bw. Kabantega alisema ni kwa sababu Bodaboda wengi hawana Elimu ya Usalama Barabarani, na kuvutana na Jeshi la Polisi, na kusababisha ajali nyingi, na kuongeza kwamba kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2018 zaidi ya ajali 800 za Bodaboda zilitokea nchini na Mkoa wa Kagera ukichangia katika ajali hizo.

Katika Mkutano huo Brig. Jen. Gaguti na Bodaboda waliazimia yafuatavyo: Kwanza, Mkuu wa Mkoa Gaguti awe Mlezi wa Bodaboda Mkoani Kagera na Bodaboda waliopo mjini Bukoba wawe tayari kuufanya usafiri wa Bodaboda kuwa wa kuaminika, kwa kufuata sheria na kuvaa sare, ili kuufanya mji wa Bukoba kuwa Mji wa kitalii katika suala la bodaboda.

Pili, Bodaboda wavae viaksi mwanga (Reflectors), vyenye namba na eneo Bodaboda, anakofanyia kazi, ambapo Mkuu wa Mkoa aliwaahidi Bodaboda walioudhuria mkutano huo, kuwapa bure viaksi mwanga hivyo.

Tatu, kila Bodaboda kukubali kujiunga katika kikundi na kupewa elimu ya ujasiliamali, ili wakopesheke kupitia vikundi, ambapo Mkuu wa Mkoa, aliahidi kuchangia Pikipiki tatu katika vikundi vitakavyofanya vizuri, ili zawadi hizo za pikipiki ziwasaidie wanakikundi kukuza mtaji wa kikundi husika.

Naye Bw. Abdusalum Mashankara, akimshukuru Mkuu wa Mkoa kwaniaba ya wenzake, alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Gaguti kaweka historia, kuamua kuwaita na kukaa nao, na kwa kukubali kuwa mlezi wa Bodaboda katika Mkoa wa Kagera.

Bw. Mashankara alisema kuwa Mkuu wa Mkoa amewafungua macho Bodaboda, kwani kila Taasisi ina chombo chake mahala pa kupeleka kero, lakini Bodaboda hawakuwa na chombo, na kwa mwongozo wa Mkuu wa Mkoa, chombo hicho kitaundwa.

 Mwisho Bw. Mashankara alitoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Gaguti, kuwa iundwe Kamati ya Bodaboda Mkoa, ili kuweka taratibu na kanuni za kusimamia usafiri na usafirishaji wa Bodaboda hao, kuwa mzuri.

Na Sylvester Raphael

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU 2024/2025 WAFANYIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE NGARA MJINI

    May 07, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA ABUBAKARI MWASSA AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDEKEO WILAYA YA NGARA

    May 03, 2025
  • MHE HAJJAT FATMA MWASSA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA NGARA

    May 02, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA MWASSA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZAFANA KIMKOA WILAYA YA NGARA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa