- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatuma Mwassa, amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kuilinda heshima ya Kagera na Taifa kwa ujumla, hususan katika kipindi cha Uchaguzi na baada ya uchaguzi, kwa kudumisha amani na kuonesha uzalendo wa hali ya juu.
Akizungumza Desemba 18, 2025, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Ijuka Omuka 2025 sambamba na Dua na Sala ya Kuliombea Taifa, Mkuu wa Mkoa alisema Kagera imeendelea kuwa mfano wa kuigwa kitaifa katika kulinda amani.
“Niwashukuru sana wana Kagera; mlionesha uzalendo mkubwa katika kipindi chote tulichopita kama Taifa. Hamkushiriki kwa namna yoyote katika vitendo vya uvunjifu wa amani,” alisema.
RC Mwassa aliwasihi wananchi kuendelea kuwa mabalozi wa amani kwa Watanzania wengine, akisisitiza kuwa historia ya Kagera imejaa mafunzo makubwa kutokana na nyakati ngumu ilizowahi kupitia.
“Tumepitia Vita ya Kagera ya mwaka 1978, maambukizi ya UKIMWI, kuzama kwa Meli ya MV Bukoba, tetemeko la ardhi na ajali ya ndege. Haya ni majonzi makubwa, hatutamani yajirudie tena,” alisisitiza.
Aidha, alisema Tamasha la Ijuka Omuka 2025 linalenga kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani Kagera, kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kuimarisha mshikamano kupitia Bonanza la Michezo, pamoja na kuenzi utamaduni wa Kagera ikiwemo vyakula vya asili.
Kwa upande wake, akitoa salamu kwa niaba ya viongozi wa dini, Askofu Ayubu Silivester, Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Kagera (CPCT), aliwahimiza wasomi, wataalamu na wawekezaji kuikumbuka Kagera kama nyumbani na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya mkoa huo.
Tamasha la Ijuka Omuka 2025 limeanza rasmi Desemba 18, 2025, mjini Bukoba, na linatarajiwa kuhitimishwa Jumapili, Desemba 21, 2025, likibeba kaulimbiu isemayo


“IJUKA OMUKA WEKEZA KAGERA, IRUDISHE KATIKA UBORA WAKE (Make Kagera Great Again)"
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa