- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
8/07/2025
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Bi Jenifer J. Mapembe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu alifungua mafunzo elekezi kwa watumishi ajira mpya 2024/2025 katika ukumbi wa St. Francis Ngara Mjini.
Kaimu huyo Bi Jenifer amemshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa wilaya kuletewa watumishi kwa idara Mbalimbali zaidi ya 230 kwa mwaka 2024/2025.
Aidha Bi Jenifer alieleza kuwa Mafunzo hayo ni takwa la kisheria ambayo yamebainishwa kwenye kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 kifungu G.1(8).Alifafanua kwamba Watumishi hao watapata Nasaha toka kwa viongozi wa Serikali Kuu ambao ni Katibu Tawala wilaya, kamanda wa TAKUKURU , Afisa Uhamiaji na Usalama wa Taifa pia Serikali za Mitaa ( wakuu wa Idara)
Bi Jenifer alisema mada mbalimbali zitafundishwa na wakufunzi mahili toka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo aliendelea kwa kutaja mada zitakazo fundishwa ambazo ni
1.Mfumo wa Serikali za Mitaa.
2.Sheria zinazosimamia utumishi wa UMMA ,HAKI NA WAJIBU KWA MTUMISHI.
3.Maadili ya Mtumishi wa UMMA
4.Taratibu za kiofisi ,usimamizi wa kumbukumbu na Mawasiliano katika utumishi wa UMMA,
5.Usimamizi wa utendaji katika utumishi wa UMMA (PEPMIS)
6.Huduma kwa Mteja
7.Masuala Mtambuka ( uongozi na utawala bora ,mapambano dhidi ya Rushwa, mazingira , UKIMWI mahala pa kazi na masuala ya kijinsia)
Baada ya maelezo hayo Bi Jenifer aliwataka washiriki wote kuwa wasikivu na kuhakikisha wanazingatia yote yatakayofundishwa kisha alifungua rasmi Mafunzo hayo.
Kaimu Ded Bi Jenifer Mapembe akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi ajira Mpya 2024/2025
Watumishi Ajira Mpya wakiwa kwenye mafunzo Elekezi katika ukumbi wa St francis Ngara Mjini
Katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani A. Lukali akitoa Nasaha kwa watumishi waajiriwa wapya 2024/2025
Mkufunzi toka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo akifundisha watumishi wa ajira mpya katka ukumbi wa St francis Ngara Mjini.
Mwl Mkude akiongea na watumishi ajira mpya katika ukumbi wa st francis Ngara Mjini
Kamanda wa Takukuru wilaya Ndg Ally Mikidadi akitoa mafunzo dhidi ya Rushwa
Afisa elimu Msingi Mwl James Ling'hwa akitoa Nasaha
Kaimu Ded Bi Jenifer Mapembe akiongea na wanamafunzo kulia ni katibu Tawala wilaya Bi Hatujuani A Lukali na kushoto ni Ndg Bahati Marco Afisa Utumishi
Mganga Mkuu Wilaya Dr Deogratias Mlandali akitoa Nasaha
Wawezeshaji toka chuo cha serikali za mitaa Hombolo
Mwezeshaji mafunzo ndg Kweyamba Maxmilian kutoka chuo cha Hombolo akiwa na Dr David S Mapunda
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa