- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATE
14/03/2025
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Baraka Leonard alimtembelea Mhe Col Mathias Julius Kahabi Dc Ngara na kufanya naye mazungumzo ofisni kwake.
Viongozi wengine waliohudhuria Mazungumzo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mratibu wa shughuli za Mbunge Ndg. Mathias Mugata Pamoja na Viongozi waandamizi wa Ofisi ya Katibu wa Bunge.
Mhe Katibu wa Bunge pamoja na mambo mbalimbali aliyozunguza katika Kikao hicho kifupi alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Ofisi ya DC, Ofisi ya Mbunge pamoja na Viongozi wa Chama wa Wilaya.
Aidha, Mhe Baraka alisisitiza ushirikino huo uendelee kwa lengo la kudumisha utulivu mzuri wa Kisiasa uliopo ndani ya Wilaya ya Ngara na kuwaletea wananchi Maendeleo chanya ambayo Mhe Dr Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayepigania kwa nguvu zake zote.
Mhe Baraka Leonard Katibu wa Bunge akiwa katika picha ya pamoja na Col. Mathias Kahabi Dc Ngara
Mhe Col Mathias Kahabi wakiwa katika kikao kifupi na Katibu Wa Bunge pamoja na viongozi Mbalimbali
Picha ya pamoja ya Mhe Baraka Leonard katibu wa Bunge, Mhe Col Mathias Kahab Dc Ngara, Ndg Jawadu Yusufu Afisa Tarafa Nyamiaga na kaimu Das , ndg Ally Mikidadi Kamanda Takukuru wilaya , Afirican Mkude DSO , kamanda Kisaka mwakilishi Ocd na Ndg Mathias Mugatha mratibu shughuli za Mbunge
Ngara Kazi inaendelea.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa