- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
04/08/2025
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara Ndg. Constantine F. Msemwa ambapo mafunzo yatafanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 04/08-6/08/2025. Aidha Mafunzo hayo yamehudhuliwa na Ndg Laban Leonard Idefonce kutoka Tume huru ya Taifa ya uchaguzi , Wasimamizi Wasaidizi Jimbo Ndg Telesphod Ngerangera, Josephati Sangatati , Josephina J. Lusatira ,Afisa Uchaguzi Jimbo Bi Sakina Chamiti, Afisa ugavi na Manunuzi Ndg Jacob Sona , Maafisa TEHAMA Ndg. Emmanuely Ntamalengero na Ndg Shabani kimokole.
Mafunzo hayo yameshirikisha ARO Kata Wawili kila kata Jumla Wakiwa 44 kwa kata 22.
Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Msimamizi wa uchaguzi Jimbo Ndg Constantine Msemwa Ambapo alisisizita yafuatayo:
1.kusoma kwa umakini katiba ,Sheria ,kanuni,Miongozo na Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na kuuliza ili kupata kufafanuliwa kwa mada zitakazofundishwa.
2.Vishirikishwe vyama vyote vya Siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya katiba ,sheria ,kanuni na maelekezo mbalimbali ya Tume.
3,Amewataka wajitahidi na wajiepushe kuwa vyanzo vya Malalamiko kutoka kwa vyama vya Siasa na wadau wa uchaguzi .amesisitiza kuzingatia ipasavyo katiba,Sheria ,kanuni , miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume.
4.Wawashirikishe wadau wa uchaguzi hususani katika maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ,kanuni, sheria ,Miongozo na Maelekezo ya Tume.
5 Utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini Mahitaji maalum ya vituo husika na kuhakikisha kunanakuwa na mpangilio mzuri ambao utahusu uchaguzi kwa amani na utulivu.
6.kupokea vifaa vya uchaguzi kutoka Tume na kuhakiki na kuhakikisha vinasambazwa kwa vituo vyote na kila Mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika Mapema.
7.Wakati wa kuapisha Mawakala watoe taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria ,kanuni na maelekezo ya Tume.
8, kuhakikisha siku ya uchaguzi wanaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1,00 kamili asbh na
9.kufanya Mawasiliano na Msimamizi wa uchaguzi au Afisa Uchaguzi pale ambapo ushauri utahitajika kuhusiana na masuala ya Uchaguzi
Baada ya kusisitiza hayo alifungua rasmi Mafunzo.
Mada zilizofundishwa ni
1.Majukumu ya Watendaji na Mambo Muhimu ya kuzingatia ambapo mada hii iliwasilishwa na Bi Sakina Chamiti Afisa uchaguzi Jimbo
2.Uteuzi wa Wagombea mada iliowasiliswa na Ndg Telesphord Ngerangera Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Jimbo.
3.Maadili na kampeni za Uchaguzi iliwasilishwa na Ndg Josephat Sangatati Msimamizi wa msaidizi wa uchaguzi Jimbo.
4.Wajibu na Majukumu ya Watendaji wa vituo na Utambulisho wa Mawakala wa vyama vya Siasa ambapo mada hii iliwasilishwa na Bi Josephine J. Lusatira Msimamizi Msaidizi uchaguzi Jimbo.
Mafuzo yaliahirishwa na Mkiti wa mafunzo mpaka siku ya pili Tarehe 05/08/2025.
" Kura yako ,Haki yako , jitokeze kupiga kura"
Mhe Terrysophia Tesha Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Ngara akiwaapisha Wasimamizi Wasaidizi Ngazi ya kata Jimbo la Ngara
Ndg Telesphord Ngerangera akiwezesha mada ya uteuzi wa wagombea
Washiriki wa Mafunzo wasimamizi wasaidizi Ngazi ya kata jimbo la Ngara Wakiapa
Ndg Laban L. Edefonce kutoka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi akiongea na wanamafunzo katika ukumbi wa Community Centre Ngara Mjini
Mgeni Rasmi Ndg Constantine Msemwa Msimamizi Wa uchaguzi Jimbo la Ngara katika picha ya pamoja Baada ya Ufunguzi.
Bi Sakina Chamiti Afisa Uchaguzi Jimbo la Ngara akiwezesha mada ya kwanza ambayo ni majukumu ya watendaji na mambo muhimu ya kuzingatia
Washiriki wa mafunzo wakisikiliza Mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Ndg Josephat Sangatati
Ndg Josephat Sangatati Akiwezesha mada ya Maadali na kampeni za Uchaguzi
Bi Josephat Lusatira akiwezesha mada ya Wajibu na Majukumu ya Watendaji wa vituo na utambulisho wa mawakala wa vyama vya siasa
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa