- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
01/08/2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon O. Kimilike amefanya kikao kazi na Watumishi waliopo Makao Makuu ya Halmashauri. Akifungua kikao kazi hicho alisisitiza watumishi kuwa na mahusiano mazuri kazini, upendo, ushirikiano na kufuata Sheria, Kanuni na taratibu.
Katika kikao hicho Mada mbalimbali ziliwasilishwa kama ifuatavyo:-
1) Taarifa ya Utekelezaji wa Idara ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu iliyowasilishwa na Mkuu wa wa Idara hiyo Bi. Jenifer Mapembe.
2) Elimu kuhusu Kanuni za Maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa umma za mwaka 2023 ilitolewa ambapo mada hiyo iliwasilishwa na Mkuu wa Idara ya utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Bi Jenifer Mapembe.
3) Elimu na Ufafanuzi kuhusu Muundo wa Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa (Organization structure) ıilitolewa.
4) Umuhimu wa mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa Majukumu ya kila siku katika utumishi wa Umma ambapo mada hiyo iliwasilishwa na afisa TEHAMA Ndg Shaban kimokole.
5) Matumizi ya mfumo wa Employee self Services( ESS) katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya utumishi ambayo iliwasislishwa na Ndg Boniface Mwakikuti na Bi Jasmine. kutoka Ofisi ya Mipango.
6) Masuala mbalimbali ya kiutumishi ambayo ni Mawasiliano, kuwahi kazini, kukaa sehemu ya kazi, utoro wa rejareja, Rushwa mahala pa kazi, utunzaji wa SIRI na utaratibu wa Ruhusa na likizo.
7) Mada kuhusu changamoto za Afya ya akili kwa watumishi iliwasilishwa na Afisa ustawi wa Jamii Ndg. Balongondoza.
8) Elimu kuhusu Bima ya Afya pamoja mfumo wa Bima ya Afya wa NHIF Self Service ilitolewa na Mtaalamu kutoka Ofisi ya Bima ya Afya Bukoba.
9) Baada ya mada hizo yalifanyika majadiliano mbalimbali ambapo hoja zilizoibuka zilitolewa majibu na Ufafanuzi na pia maoni na mapendekezo mbalimbali yalitolewa.
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg Solomon Kimilike aliahirisha kikao kazi hicho cha watumishi wa Makao makuu ya Halmashauri kwa kusisitiza yafuatayo:-
i) Utendaji kazi wa Halmashauri ufanyike kwa kuzingatia Mkataba wa huduma kwa Mteja.
ii) Utunzanji wa Siri za Serikali ni jambo la Msingi na lizingatiwe.
iii) Watumishi wakae ofisini wafanye kazi na waache Majungu.
iv) Haki itolewe bila upendelea kwa watumishi wote.
vi) OC za Idara zitumike vizuri ikiwemo kulipa stahiki mbalimbali za watumishi.
viii) Watumishi wafike kazini kwa wakati na kuwe na Movement Register ya watumishi wanaotoka nje ya Ofisi wakati wa kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wilaya Ndg Solomon Kimilike alipokuwa akifungua kikao kazi cha watumishi kushoto ni Mkuu wa idara ya Utawala na rasilimali watu Bi Jenifer Mapembe
Bi Jenifer Mapembe Mkuu wa Idara ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali wayu alipokuwa akiwasilisha mada tatu katika kikao kazi.
Watumishi wa Makao makuu wakiwa kwenye kikao kazi
Watumishi wakiwa kwenye kikao kazi cha Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa