- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
09January 2024
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja aliongozana na Afisa elimu Sekondari Mwalimu Enock Ntakisigaye, kaimu Afisa Elimu Msingi Mwalimu Ezekiel Nzabhayanga na Afisa Mawasiliano Serikalini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra C. Mwankenja Ametembelea na kukagua shule Mbalimbali za Awali, Msingi na Sekondari ili kuona Hali ya mapokezi Kwa wanafunzi katika shule za Msingi Nzaza, Shule ya Msingi Kabanga, shule ya Sekondari Kabanga, shule ya Msingi Ngara Mjini, shule ya Sekondari Ngara.
Nae Afisa Elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye akiwa shule za sekondari Kabanga na Ngara Sekondari amewataka wazazi kuwapelekea wanafunzi wa kidato Cha Kwanza kuripoti hata kama wanamapungufu watapokelewa tu kamwe asitokee mkuu wa Shule yeyote ya Sekondari kutompokea mwanafunzi Kwa sababu ya mapungufu ya aina yetote
Naye kaimu Afisa elimu Msingi mwl Ezekiel Nzabhayanga aliwaasa wazazi wawapeleke watoto shuleni alisisitiza kuwa Elimu ni ufunguzi wa Maisha tuwapeleke watoto akiwa shule za Msingi Nzaza, kabanga, na Ngara mjini aidha walimu watimize wajibu wao kuwafundisha watoto Kwa kufuata Ratiba il noti kuepuka upotevu wa vipindi usio na tija.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja akiwa kwenye shule za Msingi na Sekondari akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Kabanga amewapongeza wanafunzi hao Kwa kuripoti ndani ya muda uliopangwa. Aidha Amewasihi wazazi ,walezi kuhakikisha Kila mwenye Mtoto wa kuanza Madarasa ya Awali, shule ya Msingi na waliofaulu kuingia kidato Cha Kwanza wahakikishe wanawapeleka watoto shule,Kwani Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekamilisha miundombinu yote inayohitajika ikiwa tayari Kwa kupokea wanafunzi.
Wanafunzi wa kidato Cha Kwanza walioripoti shule ya Sekondari Ngara na wanaendelea na mapokezi shuleni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja, Afisa elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye, Kaimu Afisa elimu Msingi Mwl Ezekiely Nzabhayanga wakiwa na wanafunzi wa kidato Cha Kwanza na Wazazi waliofika shule ya Sekondari Kabanga waliofika kuripoti.
Wanafunzi wa Darasa la kwanza walioripoti shule ya Msingi Kabanga Sekondari wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja akiwa na Afisa elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye na kaimu Afisa elimu Msingi Mwl Ezekiel Nzabhayanga.
Wanafunzi kidato Cha Kwanza walioripoti kidato Cha Kwanza Ngara Sekondari wakiwa na viongozi wa Halmashauri.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bi Sabra Mwankenja akiongea na walimu Shule ya Sekondari Ngara akiwa na Afisa elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye , kaimu Afisa elimu Msingi Mwl Ezekiel Nzabhayanga na Mkuu Wa Shule Ngara Sekondari Mwl Daudi Marco.
Pia viongozi wamezungumza na walimu Shule ya Ngara Sekondari.
Walimu wa shule ya Sekondari kabanga.
Walimu Shule ya Ngara Sekondari.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa