- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe. Lt.Col. Michael Mangwela Mntenjele amezindua rasmi zoezi la kupiga chapa mifugo hasa ng’ombe walioko ndani ya wilaya ya Ngara. zoezi hilo kiwilaya limefanyika katika kijiji cha Kasulo kata ya ya kasulo.
Kabla ya uzinduzi kufanyika Mkuu wa wilaya amewahutubia wananchi na wafugaji waliohudhuria katika zoezi hilo na kueleza faida za kufanyika kwa zoezi la kupiga chapa mifugo, kwanza ni kutambua wafugaji na mifugo yao. Pili, kudhibiti wizi, utoroshaji na uhamishaji horera wa mifugo kutoka eneo moja kwenda jingine. Tatu, kusaidia kupunguza migogoro baina ya wafugaji na wafugaji, na baina ya wafugaji na wakulima nan ne, kuwa rahisi kupanga mipango ya maendeleo ya mifugo.
Aidha amesisitiza kuzingatia sheria ya wanyama ya mwaka 2013 ambapo mifugo ikishasajiriwa haipaswi kutoka mahali iliposajiriwa kwenda eneo jingine. Pia amekazia kuzingatia sharia ya maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo namba 13 ya mwaka 2010 ambayo inakataza kuingiza mifugo ya kutoka nje ya nchi na kuichunga hapa nchini.
Amewaomba wananchi kutoogopa kutoa taarifa za mifugo ambayo si ya wilaya ya Ngara, lakini pia kutoa taarifa za mifugo inayopelekwa kwenye maeneo ya hifadhi.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W), Ndg Gedeon Mwesiga ameeleza kuwa wilaya ya Ngara inategemea kupiga chapa ng’ombe Zaidi ya elfu sabini na tano (75,000) kupitia zoezi hili ambalo linaratibiwa na idara ya Mifugo na Uvuvi.
Kaimu Mkurugenzi pia ameeleza kuwa ofisi yake kupitia idara mama ya zoezi hili (Idara ya Mifugo na Uvuvi), serikali za vijiji na uongozi wa kata, imejipanga kuhakikisha mifugo yote itakayopigwa chapa ni ya wilaya ya Ngara na si vinginevyo. Ametoa rai kuwa atakayehusika na udanganyifu wowote katka zoezi hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa