- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Zoezi la oparesheni sikiliza na kutatua kero pia kukagua Miradi ya Maendeleo limeendelea katika Kata ya Kanazi ikiongozwa na Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara akifuatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg Solomon Kimilike aliyewakilishwa na Afisa Elimu Secondary Ndg Enock Ntakasigaye, Kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Taasisi(TARURA, RUWASA, TANESCO na NIDA), wakuu wa Idara na vitengo vya Halmashauri, Viongozi wa Kata akiwemo Mhe. Sitini Elphas- Diwani Kanazi na viongozi wa Vijiji na Uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii - Lemela.
Mhe Mkuu wa wilaya walitembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Kata hiyo ikiwemo Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Lemela, zoezi la Upandaji wa nyasi katika uwanja Michezo uliopo lemela ambao unasimamiwa na LADP na kugharimu kiasi cha TSh Milion 23. Ujenzi wa vyumba vya Madarasa viwili Shule ya Secondary Kanazi unaogharimu kiasi cha TSh Milion 50 pamoja na matundu manne ya vyoo katika Shule hiyo utakaogharimu kiasi cha TSh Milion 8.4.
Mhe Col.Kahabi Amemshukuru na Kumpongeza Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutuma fedha nyingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ambayo inatekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Sekta mbalimbali za Elimu. afya, Umeme, Barabara na Maji.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa