- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu na wanafunzi wa darasa la saba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa wasibweteke kwa matokeo mazuri ya mtihani wa Mock wa mkoa wa Kagera, badala yake waongeze jitiada ili wafanye vizuri zaidi katika mtihani wa taifa.
Hayo ni kwa mujibu wa Afisaelimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Idara ya Elimu Msingi ndugu Gideon Mwesiga, wakati alipokuwa akijumuisha matokeo hayo kwa ajili ya kuyapeleka mkoani Agosti 03, 2018.
Ndugu Mwesiga amesema kwamba wanafunzi waliofanya mtihani huo, wavulana walikuwa 2,344 na wasichana walikuwa 2,680, ambapo jumla ya watahiniwa walikuwa 5,024 na kwamba waliofaulu walikuwa 4,991 sawa na 98.28%.
“Ninaloweza kusema hapa walimu waongeze juhudi, na watahiniwa waongeze juhudi za kusoma wasibweteke kwa kufaulu mithani wa mock wa mkoa, huku nikiwa na furahi kwa ufaulu wetu kupanda kwa 6.25% ikilinganishwa na ufaulu wa mithani wa Mock wa Wilaya.” Alisema Afisaelimu Ndugu Mwesiga.
Amesema baada ya matokeo hayo walimu, wameonyesha hari ya kufundisha na wanafunzi wameongeza bidii zaidi wakionyesha nia ya kupunguza dosari, ambazo zimejitokeza katika mithani wa mock, wakilenga kufanya vizuri katika mtihani wao wa taifa.
Hata hivyo, alizitaja changamoto zilizojitokeza katika mtihani wa mock wa mkoa, kuwa ni kusiliba kusikotakiwa; huku akiwataka walimu wa masomo, wakuu wa shule na waratibu kata kuhakikisha watahiniwa wanapewa mazoezi zaidi ya kusiliba kabla ya mtihani wa taifa.
Amehimiza walimu kutumia mbinu ya kuwafundisha watoto hao kwa pamoja (team teaching) kwa shule za jirani mbili au tatu ili wabadilishane ujuzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara katika mwaka wa 2018 ina watahiniwa wapatao 5,095 wavulana wakiwa 2,391 na wasichana ni 2,704 waliosajiliwa kufanya mithani wa taifa wilayani humo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa