- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Eng. kundo Andrea Mathew Amefanya ziara Wilayani Ngara aliongozana na Wahandisi Toka wizarani, Meneja wa TTCL Mkoa, Afisa Habari Mkoa kagera ambapo amekagua Mkongo wa Mawasiliano eneo na Rusumo kata ya Rusumo Tarafa ya Nyamiaga Wilayani Ngara.
Aidha Naibu Waziri huyo Mhe Eng Kundo baada ya kukagua Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa Uliopo kata ya Rusumo amefanya Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Rusumo eneo la ofisi ya Kijiji Cha Rusumo.
Mhe Naibu Waziri alipokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias J. Kahabi na Diwani wa kata ya Rusumo ambaye pia Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara, Mbunge Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba Ruhoro ,kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Joseph Sangatati, kamati ya Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri.Viongozi wa chama na serikali akiwemo Mkiti wa ccm Wilaya Mhe Vitaris Ndailagije.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J Kahabi alitoa taarifa ya Wilaya Kwa naibu Waziri wa habari ,mawasiliano na Teknolojia.
Akiongea katika Mkutano wa Hadhara Naibu Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amewaasa wananchi kutumia mitandao Kwa manufaa yao. Aidha amempogeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa Fedha za kujenga Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Ngara pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Kwa kusimamia Miradi Mbalimbali.
Mhe Eng Kundo Methew alitoa nafasi ya kuongea kwa wananchi Kwa viongozi ambao ni Mkiti wa Halmashauri ambaye ni Diwani wa Kata hiyo ya Rusumo Mhe Wilbard Bambara pia Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G. Ruhoro ambapo Kila Moja alimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta fedha za kujenga Miradi ya maendeleo wilayani Ngara.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Julius Kahabi akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G.Ruhoro ,pamoja na Mkiti wa ccm Wilaya Mhe vitalis Ndailagije na viongozi Mbalimbali katika Mkutano wa wanachi ulifanyika kata ya Rusumo Wilayani Ngara.
Viongozi Mbalimbali katika Mkutano wa Hadhara ulifanyika kata ya Rusumo.
Mbunge wa Ngara Mhe Ndaisaba Ruhoro akiongea na Wananchi wa Rusumo katika Mkutano wa Hadhara wa Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia.
Wananchi wa Rusumo Wilayani Ngara walivyojitokeza kumpokea Naibu Waziri wa Habari ,mawasiliano na Teknolojia Mhe Eng kondo A. Methew.
Mapokezi ya Naibu Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia Rusumo Wilayani Ngara.
Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa uliotembelewa na Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Kundo Andrea Mathew.
Wananch walivyojitokeza katika Mapokezi ya Naibu Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kata ya Rusumo Wilayani Ngara.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Kanali Mathias J Kahabi akitoa taarifa Kwa Mhe Eng Kundo A.Mathew Naibu Waziri wa Habari ,mawasiliamo na Teknolojia ya Habari.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa