• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

SAMIA INFRASTRUCTURE BOND: MPANGO MADHUBUTI UWEZESHAJI WAKANDARASI WAZAWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

Wakati ilipowekwa: July 1st, 2025

DODOMA.

Wakandarasi wa ndani (wazawa) sasa wanapata mtaji kwa urahisi ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa wakati na kwa ufanisi.

Mtaji huo wanaupata kupitia hatifungani maalum iliyoanzishwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB.

Hatifungani hio ya kwanza katika sekta ya miundombinu nchini lengo lake ni kuwezesha utekelezaji wa miradi ya barabara vijijini na mijini kupitia ushiriki wa wakandarasi wazawa. 

Jina lake ni Samia Infrastructure Bond, ilizinduliwa rasmi Novemba 29, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Mhasibu Mkuu wa TARURA, CPA Jacob Nyaulingo, amesema katika mahojiano haya maalum kwamba,

Wazo la kuanzisha hatifungani hiyo lilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

"Awali lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi bilioni 150 lakini kutokana na mwitikio mkubwa kutoka kwa watanzania wa kuunga mkono juhudi hizi hali iliyopelekea kuvuka lengo hilo la ukusanyaji kutoka bilioni 150 hadi kufikia shilingi bilioni 323 sawa na asilimia 215.4 ya matarajio," amesema.

Hatifungani hiyo ina riba ya asilimia 12 kwa mwaka na fedha zilizopatikana zimeelekezwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi ya barabara chini ya TARURA.

"Ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinawafikia wakandarasi kwa haraka na bila urasimu, mfumo maalum wa kidijitali uitwao Samia Infrastructure Portal umeanzishwa," amesema.

Ameongeza "Portal hiyo, iliyoundwa na TARURA kwa kushirikiana na CRDB, inawawezesha wakandarasi kuwasilisha maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao.

"Mfumo huu huondoa usumbufu wa kusafiri na kusaini nyaraka katika ofisi mbalimbali za TARURA na benki.

"Badala yake, wakandarasi hujaza maombi mtandaoni, ambayo hupelekwa moja kwa moja TARURA mkoa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kutumwa CRDB kwa hatua za mwisho za kifedha,".

Kwa mujibu wa CPA Nyaulingo, mfumo huu umeandaliwa kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwazi katika mchakato wa mikopo.

Amesema miongoni mwa bidhaa zinazopatikana kupitia mfumo huu ni pamoja na Bid Guarantee, Performance Guarantee, Advance Payment Guarantee, Retention Guarantee, Certificate Discounting na huduma mpya kabisa ya Bridge Financing, inayolenga kumpatia mkandarasi mtaji wa haraka kabla ya malipo ya mkataba.

Katika hatua ya kuwezesha wakandarasi zaidi, CRDB imeamua kutoa mikopo hiyo bila dhamana, huku ikitoza riba nafuu chini ya asilimia 15 kwa mwaka kwa wakandarasi wanaolipa kwa wakati.

“Tunatoa wito kwa wakandarasi wote nchini kutumia fursa hii adhimu. Ni wakati wa kutekeleza miradi ya barabara kwa ufanisi, kwa wakati, na kwa kutumia teknolojia bora inayowezesha upatikanaji wa fedha kwa haraka". 

"Kupitia mfumo huu, tunaamini kuwa sekta ya miundombinu itapiga hatua kubwa na kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa,” amesema CPA Nyaulingo.

Amesisitiza mpango huu wa hatifungani unadhihirisha dhamira ya serikali katika kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi, kuharakisha maendeleo ya barabara na kuinua kipato cha wazawa kupitia fursa halisi za utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • SAMIA INFRASTRUCTURE BOND: MPANGO MADHUBUTI UWEZESHAJI WAKANDARASI WAZAWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

    July 01, 2025
  • MAJALIWA AZINDUA MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 12.4 KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO

    June 26, 2025
  • MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYIKA KITAIFA DODOMA

    June 17, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UFUNGUZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa