- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
6/01/2025
Serikali kupitia Mradi wa Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imeendelea kutoa mafunzo kwa walimu wa sekondari wanaofundisha masomo ya sayansi na hisabati 40,000 ili kuwapatia mbinu, maudhui na matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Mradi wa SEQUIP unatekelezwa kwa pamoja kati ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na unalenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2026.
Akifungua mafunzo hayo ya siku tano kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Atupele Ambwene katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera leo Januari 6, 2025, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Emmanuel Shindika amesema mafunzo hayo yataimarisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi na walimu pamoja na Wathibiti ubora kufanya tathmini ya masomo hayo nchini.
Amefafanua kuwa hadi kufikia mwezi Desemba 2024, jumla ya walimu 29,328 wamekwishapatiwa mafunzo hayo na katika awamu hii jumla ya walimu 7,940 Wathibiti ubora wa shule 159 kutoka katika mikoa 18 ya Tanzania Bara watapatiwa mafunzo hayo.
Naye, Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, Michael Ligola akitoa maelezo ya awali amewaasa washiriki kuzingatia mafunzo wanayopewa ili yakawasaidie katika ufundishaji na tathmini huku akieleza kuwa kwa mwaka 2024 Mkoa huo umeongeza kiwango cha ufaulu ambapo kidato cha sita ufaulu ulikuwa asilimia 100, kidato cha nne (82%), kidato cha pili (72%), darasa la saba (72%) na darasa la nne (84).
Awali, Mratibu Msaidizi Mradi wa SEQUIP, Richard Makota amesema matarajio ya mafunzo ni kuwa na ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi na hisabati, kuongeza matumizi ya TEHAMA shuleni katika ufundishaji na ujifunzaji, kuongezeka kwa umahiri wa mwalimu katika masomo hayo na ongezeko la wanafunzi katika elimu ya sekondari ya juu, vyuo vya kati na elimu ya juu katika masomo yanayoambatana na sayansi na hisabati.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa