- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imeombwa kuziruhusu Halmashauri kuongeza akaunti maalumu itakayotumika kutunza fedha za vijana, wanawake na walemavu, ili kurahisishsa shughuli za ukopeshaji na urejeshaji wa fedha hizo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Josephine J. Rusatira ametoa rai hiyo Septemba 03, wakati alipokuwa akikagua vikundi vya vijana, wanawake na walemavu katika kata za Mabawe, Ntobeye na Rulenge.
“Ofisi ya Maendeleo ya Jamii itaweza kuratibu vizuri shughuli zake na kuweza kujua kwa urahisi madeni na faida, vikundi vinavyodaiwa na vimerejesha kiasi gani, ikiwa serikali itaruhusu kuwepo kwa akaunti maalumu kwa ajili hiyo.” alisema Bi Rusatira.
Amesema ofisi yake inapata shida hata jinsi ya kuwawajibisha wanavikundi wasiotii taratibu za kuresha fedha waliokopa, kwa sababu mikataba haielezi wasiorejeshwa watawajibishwaje.
Ameomba kiongezeke kipengele cha kuvichukulia hatua za kisheria vikundi vyote, ambavyo vitashindwa kurejesha mikopo kwa wakati, na kuongeza kwamba baadhi wanakataa kurejesha kwa kujua kwamba hakuna hatua dhidi yao.
Katika kipindi cha mwaka 2018/2019 ofisi yake itaendelea kukopesha na kufanya ufuatiliaji kwa vikundi vya akina mama na vijana, ambavyo vinasuasua katika kurejesha mikopo yao, ili kubaini matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.
kadili ya afisa huyo kitendo cha wankikundi kukopa na kutorejesha kwa wakati kinawakwamisha wanavikundi wenigne wasiweze kukopa, hivyo wanakwamisha lengo la serikali la kutaka kuinua uchumi wa wanawake na vijana.
Aidha, amesema ofisi yake itaboresha mifumo ya ukusanyaji mapato, ili kuongeza kipato na kuweza kutoa asilimia 10% ya mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na walemavu kama ilivyoratibiwa na serikali.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imekuwa ikitoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake, kwa kutumia asilimia 10% ya makusanyo yake ya ndani, ili kuviwezesha kujikwamua kiuchumi na kuutokomeza umasikini uliokithiri katika jamii.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa