• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI BIASHARA-MAJALIWA

Wakati ilipowekwa: July 3rd, 2025

NGARA UPDATES

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi.

Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi.

Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

“Endeleeni kuimarisha ushirikiano miongoni mwenu, serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchagiza maendeleo, imeendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia bunifu”.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zikiwemo benki kuongeza juhudi katika kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuelewa, kutumia na kunufaika na huduma za kifedha kwa maendeleo yao binafsi na kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.

“Tukifanya haya tutapunguza wizi, upotevu wa fedha kiholela kwa sababu kila mmoja atakuwa anaweza kujua fedha yake ataipataje, ataihifadhi wapi na namna ya kutoa lakini pia wapeni wateja wenu namna ya utunzaji wa fedha”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa Finscope huduma jumuishi za fedha zimeweza kukua kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 76 mwaka 2023. “kwa mujibu wa utafiti huo, matumizi ya huduma za benki yameongezeka na kufikia asilimia 22 mwaka 2023 kutoka asilimia 17 mwaka 2017”.

Kadhalika, Mheshimiwa ametoa wito kwa taasisi zote za fedha zijenge mifumo rahisi na rafiki kwa makundi yote ya watumiaji wa huduma za kifedha.

Awali, Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa, Muwakilishi wa Askofu Dean Chadiel Lwiza ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuisimamia benki hiyo na kuwa mfano wa benki iliyoanzishwa na wazawa kwa mtaji mdogo hadi kufikia kuwa benki kitaifa. “Tunaiomba benki kuu jicho lenu liwe kali kuliko letu, itazameni hii benki”

Kadhalika, ameongeza kuwa sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji katika biashara na usimamizi mzuri za biashara. “Tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoomgizwa na Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuweka mazingira haya mazuri ya ufanyaji biashara”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Lomnyaki Saitabau amesema kuwa benki hiyo imejiweka katika nafasi bora zaidi ya kuwa benki ya kisasa, shindani na jumuishi kwa Watanzania wote hasa kipindi dunia inapoelekea kwenye zama mpya zenye msukumo wa kiteknolojia, ubunifu, na uwajibikaji wa hali ya juu.

“Kwa kufanya hivyo, tunaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.  Samia Suluhu Hassani, yenye dhamira ya kuwafikia watanzania wengi zaidi nchi nzima kupitia dira ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha (financial inclusion) na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta binafsi, tutaendelea kushirikiana na Serikali, katika ujenzi wa Uchumi wa nchi".

Naye, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande ameipongeza benki hiyo kwa hatua kuwa iliyofikiwa na benki hiyo katika utoaji huduma kwa watanzania hasa kwa kutumia fursa zilizowekwa na Serikali “Sisi Wizara ya Fedha tumeendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ufanyaji wa shughuli za kifedha, sasa wekeni mkakati wa kuifikisha benki hii maeneo mengi zaidi”.

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI BIASHARA-MAJALIWA

    July 03, 2025
  • SAMIA INFRASTRUCTURE BOND: MPANGO MADHUBUTI UWEZESHAJI WAKANDARASI WAZAWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

    July 01, 2025
  • MAJALIWA AZINDUA MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 12.4 KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO

    June 26, 2025
  • MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYIKA KITAIFA DODOMA

    June 17, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa