- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ndg Aidan John bahama ametoa taarifa ya mlipuko wa bomu uliotokea kwenye shule ya msingi Kihinga Tarehe 08 Novemba 2017. Aidha amewashukuru wote waliojitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu ndani ya wilaya yetu. Pia alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na ofisi yake kuwa ni pamoja na kushirikiana na taasisi nyingine za serikali na binafsi kuhakikisha afya za wahanga wa tukio hilo zinaimarika, kutoa ushauri nasaha kwa wanafunzi, walimu na wazazi ili kuwajenga kisaikolojia.
Tarehe 08/11/2017 saa 2.40 asubuhi kulitokea mlipuko wa bomu kwenye shule ya msingi Kihinga iliyoko kwenye kata ya Kibogora.
Bomu hilo lilipukia mbele ya chumba cha darasa la kwanza wakati wanafunzi wanaendelea na mtihani wa kufunga mwaka wa somo la kusoma. Bomu lilipolipuka mwalimu alikuwa darasani akitahini wanafunzi kwenye somo tajwa. Wanafunzi walikuwa wamejipanga mstari mlangoni nje ya chumba cha mtihani wakiingia mmoja mmoja.
Inasadikiwa kuwa bomu lililolipuka lilikuwa limebebwa na mwanafunzi Julian Trasis ambaye ni mmojawapo wa wanafunzi watatu waliofariki papo hapo. Kwa maelezo ya majeruhi, bomu hilo aliliokota akiwa njiani kwenda shuleni.
Mlipuko huo wa bomu umesababisha madhara yafuatayo:
Wanafunzi watano (5) walifariki. Watatu (3) walifariki pale pale shuleni. Wawili (2) walifia hospitalini Rulenge wakiwa wanapewa huduma. Wanafunzi wote waliofariki ni wavulana na walikuwa wanasoma darasa la kwanza (I)
Majina ya marehemu hao ni:
Wanafunzi watatu (3) (namba i – iii) ambao walikufa pale pale walizikwa siku hiyo tarehe 08/10/2017 na wanafunzi wawili (2) (namba iv na v) walizikwa tarehe 09/10/2016.
Mlipuko huo umeathiri ubaraza wa chumba cha darasa la kwanza kwa kutoboa mabati.
Kwa shughuli zote zilizofanyika, fungua kiambatanisho hiki
Taarifa ya mlipuko wa bomu katika shule ya msingi Kihinga.pdf
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa