- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
17/08/2025
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Mwenge Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ndg Stephen Mashauri Ndaki aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Hajjat Fatma Abubakari Mwassa wamefanya ukaguzi wa Miradi itakayozinduliwa/ kutembelewa/ kukaguliwa au kuweka mawe ya msingi Wilayani Ngara.
Mwenge wa uhuru Wilayani Ngara utapokekelewa siku ya tarehe 13/9/2025 katika uwanja wa shule ya Secondary Lukole na baada ya ukaguzi/ Uzinduzi/ kutembelea au kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali, Mwenge wa Uhuru utakesha katika uwanja wa shule ya Msingi Rulenge iliyopo. Mamlaka ya Mji mdogo Rulenge.
Aidha, Katibu Tawala Mkoa katika ziara hiyo alifuatana na Mratibu wa Mwenge Mkoa Ndg Yassin Mwinory na timu ya Watalaam ambapo waliungana na timu toka Wilayani ikiongozwa na Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara, Ndg Solomon Kimilike - DED Ngara, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri pamoja na Wakuu wa taasisi za Serikali Wilayani Ngara.
Kwa namna ya pekee kabisa Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara anatoa rai kwa wananchi wote wa Wilaya ya Ngara kujitokeza kwa wingi siku ya mapokez ya Mwenge wa uhuru - Lukole Secondary na katika Mkesha - Rulenge.
Mhe Steven M. Ndaki Katibu Tawala Mkoa wa Kagera akiwa na Mhe Col. Mthias J kahabi Dc Ngara . Ndg Solomon kimilike Ded Ngara na Ndg Yasini Mwinory Mratibu Mwenge Mkoa wakiwa wakiwa kwenye mmoja wapo wa mradi wa Mwenge 2025 Ujenzi wa Daraja la kumwendo
Timu ambayo imeongozwa na Ndg Steven Mashauri Ndaki Katibu Tawala Mkoa wa Kagera walipotembelea kuona Majiko ya nishati safi na Salama
www.ngaradc.go.tz
Ngara Kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa