- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 05 April 2024.
Umefanya Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji Mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi katika Ukumbi wa St Francis Ngara mjini, Ambapo Mgeni Rasmi katika mkutano huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Abubakari Mwassa kauli mbiu ikiwa ni " USAWA WA KIJINSIA KATIKA UMILIKI WA ARDHI KWA USTAWI WA JAMII"
Taarifa fupi ya mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi ilisomwa na Ndg Remigius kawishe Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya.
Katika mkutano huo Mhe. Vitalisi alitoa shukuran kwa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbuge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba J. Ruholo kwa kutambua umuhimu wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi.
Ilitolewa nafasi Kwa wenyeviti wa mitaa mbalimbali kutoa ushuhuda wa Mpango huo na baada ya ushuhuda.
Ripoti ya uwasilishaji wa utekelezaji Mradi halmashauri ya wilaya ya Ngara ilisomwa na msimamizi wa mradi - LTIP, mwakirishi wa wizara ya ardhi pamoja na Meneja uendeshaji mradi vijijini, Ikielezea mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi wilaya ya Ngara, Ikiwa ni mipango ya kamati ya ardhi ikiwa ni pamoja na
Msimamizi wa mradi - LTIP ndugu cosmas alimalizia Kwa kutoa shukuran kwa Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa kuleta fedha katika halmashauri ya wilaya ya Ngara zilizowezesha mradi huo.
Wasilisho kutoka Kwa wadau - TANAPA, lilielezea kuwa changamoto ya wanyamapori imeongezeka Kwa sababu Kuna ongezeko kubwa la mifugo ndani ya hifadhi, kuwepo Kwa makazi ndani ya hifadhi, wananchi kutokujua Sheria ya hifadhi, pia matukio ya Rushwa Kwa watumishi pamoja na wananchi ndiyo sababu kubwa inayofanya wanyamapori kuongezeka kutoka kwenye hifadhi na kukimbilia kwenye makazi ya watu na kuleta mahafa kwenye jamii.
Pia Mdau wa TANAPA Amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la kipato kupitia utalii, ikiwa ni kupata wawekezaji wapya kwenye miradi ya utalii, lakini pia alitoa gharama za kuingia kwenye hifadhi ikiwa ni kwa mtu mzima ni Tsh. 5900/ Kwa mtoto ni Tsh. 2000/= kama kuna usafiri unalipiwa gari ndogo Tsh. 20000/= na gari kubwa ni Tsh. 40000/=.
Mwisho Amesema kuwa angalau Kwa miezi kumi ameweza kupunguza uvamizi wa hifadhi za taifa ili kulinda ongezeko la wanyamapori kwenye hifadhi hizo pia ametoa shukuran kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta miradi inayolinda hifadhi za wanyamapori.
ilitolewa nafasi ya majadiliano Kwa wadau walihudhuria na maswali yote yaliyoulizwa yalijibiwa Kwa kutolewa ufafanuzi wa kina na kuwafanya wadau kuridhika, lakini pia wadau walitoa maoni mbali mbali kuhusu mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi wilayani.
Baada ya majadiliano iliazimiwa kwenye mkutano kama ifuatavyo
Mwisho imetolewa shukuran Kwa wadau wote waliohudhuria Mkutano ambapo Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Adronizi Bulindori alifunga Kwa kutoa shukrani kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajjat Fatma Mwassa pamoja na kamati nzima ya ardhi Kwa kutambua umuhimu wa Mradi huu.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajatt Fatma Mwassa akiwa katika picha ya pamoja na Mhe Mkuu wa wilaya Col Mathias Kahabi ,Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon kimilike, Mkiti wa CCM Cde Vitaris Ndailagije, Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara katika Ukumbi wa St Francis Ngara Mjini.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa