- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
9/07/2025
Yamefanyika mafunzo elekezi kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari ambapo mafunzo hayo yametolewa na Tume ya utumishi wa walimu (TSC)
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mwenyekiti wa tume ya utumishi wa walimu Mwl Niyongele Mzungu Gibson ambapo alisisitiza mambo yafuatayo
1.Uadilifu kwa kuwa mfano wa kuigwa
2.kujituma na ubunifu aliwataka kutumia rasilimali (vitabu) kwa ubunifu mkubwa
3.kujifunza muda wote kwani kuna mabadiliko mengi yanatokea kielimu.usipokuwa tayari kujifunza kujifunza utabaki nyuma ( kupitwa na wakati)
4.ushirikiano wa walimu
5 Utunzaji wa Nyaraka
Katika mafunzo hayo mada zilifundishwa ambazo ni
1.Ajira kwa walimu
2.Nidhamu na maadili ya walimu
Aidha nasaha mbalimbali zimetolewa na maafisa elimu msingi Mwl James Ling'hwa , afisa elimu watu wazima na kaimu Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya.
Katibu ya tume ya utumishi wa walimu Bi Madina korongo alizungumzia yafuatayo
1. Muundo wa Tume
2. Kazi za tume ya Utumishi
3. Dhana ya nidhamu
4. Mamlaka ya nidhamu
5. Aina za adhabu
6. Kanuni na sheria zinazotumika
7. Haki na wajibu kwa walimu
Nae Afisa ajira Bw Erick kagya amesisitiza mambo mbali yanayohusu walimu
Walimu wa shule za Msingi na Sekondari wakiwa kwenye mafunzo elekezi ukumbi wa Ngara sekondari
Maafisa wa tume ya utumishi wa walimu wakiwa na Afisa elimu Msingi Mwl James Ling'hwa kwenye mafunzo elekezi ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa