- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 20/8/2023 Uongozi wa juu wa Tembo Nickel akiwemo Mr Benedict Busunzu - CEO Tembo Nickel pamoja na Dr. Kudra Said - OHS Manager Tembo Nickel umefika ofisi ya DC Ngara, ambapo CEO alitoa taarifa fupi ya maendeleo ya mradi huo kama ifuatavyo:-
1. Mchakato wa Utoaji wa Elimu/Mafunzo na Malipo ya fidia kwa Waguswa(PAPs) wa mradi kwa Vijiji Vitano(5) vinavyoguswa na mradi huo liko katika hatua za mwisho.
2. Zaidi ya Shilingi Bilioni 32 zimetengwa kama fidia ya Waguswa wa mradi huo.
3. Baaada ya zoezi la ulipaji fidia kwa PAPs wote zoezi litakalofuata ni Zoezi la Uhamishaji Watu na Makazi kwenda maeneo mapya ambayo tayari yametengwa kwa ajili yao.
Kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Ngara, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa napenda kumshukuru na kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha hizi nyingi zilipwe haraka iwezekanavyo kwa Waguswa wote na Malipo hayo yafanyike kabla ya kuanza Zoezi la kuhamisha watu kwa ajili ya kupisha shughuli za mradi kuanza.
Pili, napenda nimpongeze sana Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Bi. Hajjat Fatma Abubakar Mwassa kwa ufuatiliaji na usimamizi madhubuti wa kuhakikisha wananchi wote wenye stahiki ya kulipwa fidia wanalipwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo. Mwisho lakini sio kwa umuhimu kwa namna ya kipekee napenda kuwapongeza sana Viongozi MR BENEDICT BUSUNZU - CEO kwa ushirikiano na Mshikamano wa hali ya juu sana katika utekelezaji wa Shughuli na kazi mbalimbali za mradi huo kwa Uongozi wa Serikali ya Wilaya na Vijiji vyote vinavyoguswa na mradi wa Tembo Nickel.
Hakika wametushirikisha vizuri katika kila hatua ya maendeleo ya miradi huo.
Mwisho, niwashukuru sana Wananchi wa Wilaya ya Ngara hususan wa vijiji vya Nyabihanga , Bugarama, Rwinyana, Mukubu na Muganza kwa ushirikiano wao mkubwa waliouonesha toka hatua za mwanzo za mradi upimaji na Uthamini na sasa hatua za mwisho za Utoaji elimu, malipo na uhamishaji wa watu na Makazi.
Ahsanteni sana wenu *Mhe. Col Mathias Julius Kahabi - DC Ngara.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa