- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe Mohammed Mchengerwa hivi karibuni amekabidhi Tuzo na Cheti zilizotolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kutokana na Usimamizi Mzuri wa Ujenzi wa shule za Secondary kwa Mpango wa SEQUIP kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Mathias Julius Kahabi kwa niaba ya Kamati ya Usalama ya Wilaya wanatoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Cde Solomon Kimilike pamoja na Wataalam wote (timu ya Wahandisi wakiongozwa na Eng. Simon Mtuka ), M/Kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe Wilbard Bambara na Baraza la Madiwani kwa usimamizi mzuri wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri yetu.
Aidha, kipekee pongezi nyingi sana zimfikie Mhe Ndaisaba George Ruhoro kwa kuendelea kuwasemea vizuri wananchi wake na Jimbo la Ngara na tunaendelea kushuhudia fedha nyingi za miradi Maendeleo zikitumwa Jimboni....
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa