- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tuesday 21st, January 2025
@Kata ya Murukulazo Wilayani Ngara Kagera.
Maadhimisho ya siku ya Mazingira kimkoa yalifanyika Kata ya Murukulazo wilayani Ngara.Ambapo Mgeni rasmi alikuwa alikuwa Mhe Mkuu wa Wilaya Col. Mathias J.Kahabi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa kagera.
Jumla ya Miti 2300 aina ya Mikaratusi na Parachichi ilipandwa katika maeneo ya shule ya Sekondari Shunga na Shule ya Msingi Murukulazo zoezi Hilo likiongozwa na Mgeni rasmi Mhe Mkuu wa Wilaya .
Miti hiyo ilitolewa na Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Solomon Kimilike miti 1200, Marafiki wa Africa miti 1000, Nmb miti 50 na Mdau Ndg Andrew I.Baliendeza miti 50 na kufanya Jumla ya Miti 2300.
Aidha Mhe Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi kufanya zoezi la upandaji miti liwe ni endelevu.pia miti ya Matunda Parachichi imepandwa Ili kupambana na utapia mlo sambamba na miti ya Mikaratusi Kwa ajili ya upatikanaji malighafi Mbao Kwa ujenzi huko mbeleni.
Kauli mbiu ikiwa "Mazingira yangu,Nchi yangu Nitaipenda"
Maadhimisho yalikwenda sambamba na burudani mbalimbali kutumbuiza wananchi
Kitengo Cha Mawasiliano Ngara DC
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa