- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura kulisimamia Jeshi la hilo kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani, kuimarisha doria (highway patrol) usiku na mchana pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye Nyumba za Ibada katika kipindi cha sikukuu za Christmass na Mwaka Mpya.
Bashungwa ametoa maagizo hayo, leo tarehe 18 Disemba, 2024 wakati akitoa taarifa kwa Umma kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka ambapo amewahakikishia wananchi na Watanzania wote kuwa nchi iko salama.
“Hatuko tayari kuacha tabia za kizembe ziendelee kupoteza maisha ya watu, na wengine kupata ulemavu, huku Sheria za kudhibiti uzembe zikiwa zipo. Tutachukua hatua kali kwa madereva na wasafarishaji wazembe. Ninaomba wasafiri mtupe ushirikiano, na kuunga mkono jitihada hizi, ili tuwe salama tunapokuwa barabarani”amesema Bashungwa
Bashungwa ametoa wito kwa wasafiri na wasafirishaji, kuzingatia na kuheshimu Sheria za Usalama Barabarani, ili kupunguza ajali zinazoepukika ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na hata kusababisha ulemavu kwa wananchi.
“Nitoe tahadhari kwa familia zinazotumia magari yao binafsi, kufanya matengenezo ya magari kabla ya safari, na kuacha utamaduni wa kuchukua mtu yeyote ambaye hana taaluma ya udereva, wala leseni, na hajapitia mafunzo ya kuendesha magari kwa kukwepa gharama. Kila familia ichukue tahadhari, hususani tunapoelekea mwisho wa mwaka.”
Aidha, Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na TANROAD pamoja na TARURA kukagua maeneo yote nchini yenye vizuizi na vituo vya ukaguzi, kuangalia kama vimewekwa kwa kuzingatia sheria, na tahadhari ya usalama kwa watumiaji wengine wa barabara na kama vipo katika maeneo hatarishi viondolewe.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa