- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
27/09/2025
limefanyika Bonanza la Michezo Mbalimbali katika uwanja wa Halmashauri Ngara Mjini.
Kabla ya Bonanza imefanyika Jogging na mazoezi ya Aerobic kwa kushirikisha watumishi na wananchi
Baada ya maxoezi ya pamoja limefanyika Bonanza kabambe kwa michezo ya Soka, Kikapu na wavu
Matokeo ya Michezo katika Bonanza hili ilikuwa kama ifuatavyo:
1. SOKA
WATUMISHI MAKAO MAKUU 2 VS WALIMU 0
Wafungaji katika Mchezo huo alikuwa Ndg Bahati Marco kutoka Utawala na Juma Ramadhani kutoka ofisi ya Ugavi
2. WAVU (VOLLEYBALL ) WALIMU 2 VS WATUMISHI MAKAO MAKUU 1
3. KIKAPU ( BASKETBALL) WATUMISHI MAKAO MAKUU 21 VS WALIMU 6
Magoli yamefungwa na Victor Mtui kutoka ofisi ya Mipango na Salum Mnundulu.kutoka ofisi ya Mazingira.
Bonanza hilo ambalo lilikuwa na lengo la kufahamiana watumishi wa makao makuu na walimu. Kujenga afya, umoja, upendo na Mshikamano ikiwa na kubadilishana mawazo baina ya watumishi kwa watumishi.
Bonanza hilo liliandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kupitia kitengo cha Utamaduni sanaa na Michezo
Wanamichezo wamemshukuru Ndg Solomon kimilike Mkurugenzi mtendaji Wilaya kwa ukarabati wa Viwanja vya michezo Wavu na kikapu.
Imeelezwa na wanamichezo kwa Mwakilishi wake Mkurugenzi Mtendaji Wilaya katika Bonanza hilo Mwl. Said Salum ambaye ni Afisa utamaduni sanaa na Michezo - Mkuu wa kitengo hicho.
Ngara kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa