- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
26/07/2025
Kimefanyika kikao kazi cha tathimini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Afua za Lishe katika ukumbi Mdogo wa Mkuu wa Wilaya na kimefunguliwa na Mwenyekiti Bi Hatujuani A Lukari Katibu Tawala Wilaya kwa niaba ya Mhe Mkuu wa Wilaya.
Kikao hicho kimehudhuliwa na Bi Vivian Maruhe Kaimu Mkuu wa idara ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu , Bi Jasmin Abas - kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na uratibu, Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo pamoja na Maafisa watendaji kata 22 za wilaya ya Ngara.
Ndg Leonard Kepa Afisa Lishe wa Halmashauri aliwasilisha taarifa za Afua za Lisha ya wilaya kwa shughuli zilizotekelezwa kwa robo ya April - June 2025.
Katika kikao hicho Mwenyekiti aliwaasa Maafisa watendaji kuhakikisha wanafuatilia afua za lishe katika maeneo yao ya kazi. Pia alisisitiza wawe wanashiriki katika siku ya Afya na Lishe kwenye vijiji vilevile aliwaasa Maafisa watendaji juu ya utoaji wa Elimu ya ulaji makundi 6 ya vyakula.
Ngara kazi inaendelea.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa