- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
05/03/2025
Mhe Col. Mathias J .Kahabi DC Ngara amefanya Mkutano wa Hadhara kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi kijiji cha Magamba kata ya Mursagamba Tarafa ya Mursagamba.
Katika kikao hicho aliongozana na K/Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya katibu Tawala Wiaya Bi Hatujuani A. Lukali, Wajumbe kamati ya usalama wilaya, wakuu wa Idara na vitengo vya Halmashauri , Wakuu wa Taasisi za serikali pamoja na uongozi wa kata na kijiji husika.
Wananchi walitoa kero zao na kutatuliwa na wakuu wa idara, taasisi za serikali
Aidha Mhe Col Kahabi amesisitiza yafuatayo
Aidha Mhe Col Kahabi amesisitiza kuwa Migogoro ya Ardhi inapoletwa isipuuzwe na ianzie Ngazi ya kijiji,kata hadi Tarafa itenge muda kuwasikiliza Wananchi na kuzitatua changamoto hizo ili jamii inufaike kupitia uwepo wao, yale yanayoshindikana Mhe DC alisema muda wote kuwatumikia wananchi,
Pia Mhe Col Kahabi amekemea vitendo vya Raia kuwaficha wahalifu huku akitoa mifano hai iliyotokea katika eneo hilo waliofichwa kwenye majumba ya watu na kutekeleza matukio mengi ya kiuhalifu
Viongozi mbalimbali kamati ya ualama wilaya, wakuu wa idara Halmashauri na wakuu wa taasisi za serikali katika kikao cha kusikilia na kutatua kero kijiji cha Magamba kata ya Mursagamba.
Wananchi wa kijiji cha Magamba kata ya Mursagamba wakiwa kwenye kikao cha kusikiliza na kutatua kero za wananchi
wananchi
Mhe col Mathias J Kahabi Dc Ngara akiongea na wananchi wa kijiji cha Magamba kata ya Mursgamba
Kazi inaendelea Ngara
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa