- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Mkuu wa wilaya Mhe Col Mathias J kahabi ameendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kijiji Cha chivu kata ya Ntobeye.
Mhe Col Kahabi alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, katibu Tawala Wilaya , kamati ya usalama Wilaya, Wataalam Kutoka Halmashauri ya Wilaya, Taasisi za Serikali Tarura ,Ruwasa,Tanesco, pia Afisa Tarafa Nyamiaga, Mhe Diwani Kata ya Ntobeye, Viongozi wa Chama na serikali Kutoka Kata hiyo.
Mhe Kahabi amesisitiza suala la amani ambapo alisema Maendeleo hayawezi kuja bila kuwa na amani ,Amehimiza wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa kuchagua viongozi wanaokubalika, pia umuhimu wa Elimu Kwa kuwataka Wazazi kuwapeleka shule watoto wasikatizwe kwani Elimu ni ufunguo wa maisha.
Aidha Mhe Col Kahabi ametembelea kuona ujenzi wa shule shikizi ya chivu na kuahidi kuwapa saruji mifuko 50 Ili kusaidia nguvu za wananchi katika ujenzi huo wa vyumba 2 na Ofisi.
Naye Mhe. Sunday mukozi Diwani Kata ya Ntobeye aliipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa Miradi ya TASAF, umeme,Barabara pia ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya sec Ntobeye, zahanati ya Kijiji Cha kigina.
Kero zilizoulizwa na wananchi ni masuala ya umeme, Barabara, maji, Elimu, Ardhi na uhamiaji.
Ambapo kero hizo zilisikilizwa na kujibiwa na wataalam aliyoambatana nao Mhe col Kahabi Mkuu wa wilaya.
Imesisitizwa wananchi wanapolipia huduma za Serikali wajiepushe kulipa fedha taslimu Bali watumie mfumo wa Malipo wa Serikali Kwa kupewa namba ya Malipo (control number)
Mhe Kanali Kahabi akihitimisha Kwa kumpongeza na kumshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa serikali anayoiongoza Kwa kuleta fedha za ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu, maji, umeme na Barabara.
Wataalam wakiwa kwenye mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mhe col Kahabi akisilikiza kero ya mwananchi.
Wananchi walivyojitokeza kwenye mkutano wa Hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mhe Diwani Kata ya Ntobeye Sunday mukozi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa