- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya Mhe Kanali Mathias Kahabi amefanya ziara Tena kukagua ujenzi wa Soko la Kahaza na kazi inaendelea baada ya Mkandarasi kukaa ndani siku mbili Kwa kuonekana Kasi ya ujenzi wa Soko hilo la Kimkakati kusua sua.
Ukaguzi wa mwanzo alioufanya Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg Solomon Kimilike, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wasimamizi wa Mradi LADP, Wataalam wa Halmashauri chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkandarasi pamoja na Viongozi wa Serikali ya kijijni cha Rusumo tarehe 23/12/2023.
Ambapo hawakuridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa mradi huo Mhe Mkuu wa wilaya Col. Kahabi alilazimika kumuweka ndani Mkandarasi kwa kushindwa kwenda na kasi inayotakiwa kulingana na Mkataba ambapo alikuwa ameshalipwa TShs Milioni 377 kama malipo ya awali (Advance Payment).
Aidha Pamoja na malipo hayo ya awali Mkandarasi hakuweza kwenda na kasi inayotakiwa ikiwemo kushindwa kuleta local and industrial materials ya kutosha kwenye eneo la mradi.
Baada ya ukaguzi huo Mkandarasi huyo alifanya commitment mwenyewe kwa Mkuu wa Wilaya Mhe kanali Kahabi na Kamati ya Usalama ya Wilaya kwamba atahakikksha mradi unaenda kwa kasi kubwa na kwamba atamaliza Ujenzi wa mradi huo ifikapo mwezi March 2024 kama ilivyo kwenye Mkataba.
Leo tarehe 13/01/2024, Mhe Col Mathias Kahabi ametembelea mradi huo akifuatana na Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalam wasimamizi wa mradi LADP, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Mkandarasi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya kijijni cha Rusumo na kuridhishwa na kasi inaendelea hivi sasa na Materials yaliyopo site, hivyo ameagiza kasi iendelee na kwamba yeye na Viongozi wenzake watakuwa wanafika angalau mara mbili kwa wiki kwa ajili ya ukaguzi wa Ujenzi wa mradi huo.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Kahabi amesema kamwe hatakubali kuona Juhudi kubwa za Mhe Dr. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinajaribu kuchafuliwa na Wakandarasi wachache wanaotaka kumrudisha nyuma Mhe Rais. Soko hilo linatarajiwa kukamlika mwezi March 2024.
Pia Mhe Mkuu wa wilaya na timu yake wametembelea Mradi wa ujenzi wa bweni, Bwalo na jengo la utawala shule ya sekondari Ngara high school.
Mafundi kazi ya ujenzi wa soko Mkakati la kahaza Rusumo Wilayani Ngara ambapo Mhe Mkuu wa wilaya alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji Ili kuona hali ya ujenzi.
Mafundi kazi ikiendelea.
Mafundi kazi ikiendelea soko Mkakati kahaza Kata ya Rusumo Wilaya ya Ngara.
Mhe col Mathias Kahabi Mkuu wa wilaya (mtu kazi )akiwa na kamanda wa Polisi Wilaya, Mtendaji wa Kijiji wakikagua ujenzi.
Mkuu wa wilaya Col. Kahabi akiwa na kaimu katibu Tawala Ndg Jawadu Yusuf, kamanda wa Polisi Wilaya,Mtendaji wa Kijiji,na Maafisa Toka LADP.
Mhe Kanali Mathias J Kahabi akiwa na viongozi mbalimbali katika ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Ngara high school.
Mhe Kanali Mathias J Kahabi akiwa na viongozi mbalimbali katika ujenzi wa bweni, Bwalo na jengo la utawala shule ya Sekondari Ngara high school (Mradi unaosimamiwa na LADP).
Mhe col. Kahabi akipata maelezo mbalimbali ya ujenzi wa bweni , Bwalo na jengo la utawala shule ya Sekondari Ngara high school.
Mhe Col. Kahabi akiwa eneo la ujenzi.
Mhe Mkuu wa wilaya amesisitiza vifaa vyote vya ujenzi viwepo site bila kukosa kwenye ujenzi wa soko la kahaza Rusumo Wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa