- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
21/01/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara katika ziara hiyo alifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, wasimamizi wa Ujenzi - Chuo cha Maendeleo ya Jamii - Lemela Ngara pamoja na Watalaam mbalimbali toka Wilayani wamefanya ukaguzi wa Ujenzi wa Chuo cha VETA, kinachojengwa Kata ya Rulenge, Tarafa ya Rulenge Wilaya ya NGARA.
Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara na KU Wilaya katika ukaguzi huo wametoa maagizo kwa Mkandarasi mshauri kuongeza kasi ya ujenzi huo na yeye mwenyewe kuwepo site muda wote ili ujenzi huo uweze kwenda kwa kasi inayotakiwa.
Mhe Col. Kahabi amesema hakuna sababu ya mradi huo kusimama kwani materials mengi yapo site kama nondo, Saruji, Mchanga na tofali. Ameagiza Mkandarasi mshauri atafutwe apatikane na aripoti Ofisi ya DC Ngara kwa ajili ya kutoa maelezo ya kina kwanini ujenzi umesimama licha ya kuwepo kwa materials yote muhimu yaliyotajwa hapo juu.
Ujenzi wa Chuo cha VETA - Ngara ulianza January 2024 na unaendelea kwa hatua mbalimbali za ujenzi. Kiasi cha bilioni 1.6 zinatarajiwa kutumika hadi mwisho wa Ujenzi huo na fedha hizo zinatolewa na Serikali kuu kwa awamu. Hadi sasa kiasi cha Shs milioni 427 zimetolewa na Serikali kuu na zinaendelea kutumika.
*Mhe Col Mathias Kahabi DC* Ngara, kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya NGARA *kwa heshima kubwa amempongeza sana Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania* kwa kuridhia kutoa kiasi kikubwa cha fedha kujengwa Chuo cha VETA - NGARA.
S
Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Dc Ngara akiwa na kamati ya Usalama wilaya eneo la ujenzi wa chuo cha VETA Ngara kinachojengwa Rulenge
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa