- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya Ngara Kanali Mathias Kahabi amewaasa bodaboda maarufu kama maafisa usafirishaji kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji kura kesho October 29, 2025 kwenye vituo vyao walivyojiandikisha ili kutimiza haki yao msingi ya kikatiba.
Kahabi ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2025 wakati akizungumza na maafisa usafirishaji wilayani humo ambapo amesema kila kijana anao wajibu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika vituo mbalimbali walivyojiandikisha ili kuhakikisha wana mchagua kiongozi atakae wasaidia kuleta maendeleo kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya huyo amewataka maafisa usafirishaji kufuata sheria na kanuni za barabarani iili kuepukana na ajali zisizokua na ulazima.



Ngara Kazi inaendelea.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa