- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
06/03/2025
DC Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi akifuatana na Mwakilishi wa DED Ndg Josephat Sangatati pamoja na Viongozi mbalimbali na watalaam toka H/W Ngara leo tarehe 06/3/2025, walitembelea S/Msingi iliyoezuliwa na upepo mkali tarehe 05/3/2025 , majira ya saa 11 jioni.
Upepo mkali uliezua madarasa mawili na ofisi ya shule hiyo ambapo watoto walikuwa wamerudi nyumbani baada ya muda wa masomo yao ya kutwa kumalizika. Hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokea zaidi ya miundombinu muhimu ya shule kuharibika ikiwemo choo ambayo iliangukiwa na paa la darasa lililoezuliwa na upepo.
Mhe DC Col Kahabi anatoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Ngara Ndg Solomon Kimilike kwa kuchukua hatua za haraka kutuma timu ya watalaam ambayo imefanya tathmini ya hasara iliyotokea na kuielekeza kuanza kurejesha miundombinu hiyo haraka iwezekanavyo.
Mhe Col Kahabi alipofika shule ya msingi Mugoma baada ya kuezuliwa akiongea na wataalam toka Halmashauri ya wilaya kufanya tathmini ya uaribifu ulitokea
Mhe Col Kahabi akiangalia uharibifu uliyotokea shule hiyo.
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa